Mwalimu wa shule ya upili huku Nthangathiri kaunti ya Embu ambaye aliripotiwa kujitoa uhai siku chache zilizopita kwa kile aitaja kwenye barua kuwa ni mapenzi, imebainika aliacha mke mjamzito.
Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyochapishwa na Taifa Leo, Dennis Mwaniki Njeru mwenye umri wa miaka 32 alijitoa uhai na kuacha sababu yake katika barua kwamba ni baada ya kukataliwa na mpenzi wake wa zamani.
Kulingana na polisi, marehemu alikuwa anavuja povu kupitia pua lake huku kemikali inayoshukiwa kuwa dawa ya kuua wadudu ikipatikana humo vilevile.
“Ni mwalimu kutoka Mbeere Kaskazini lakini anafunza katika shule ya Sekondari iliyopo Kaunti ya Kirinyaga, alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umeonyesha alijtoa uhai,” alisema.
Kwenye kijikaratasi hicho, mwendazake alisema alichukua uamuzi huo baada ya mpenziwe kumkataa.
“Naweza nikaonekana mjinga lakini nimefungua moyo wangu kuhusu kinachoniumiza kwa watu 17 lakini hakuna aliyezungumza nami, acha tukutane mbinguni. Nimemsihi mpenzi wangu lakini yote yameambulia patupu. Nawapenda nyote,” alisema kupitia barua hiyo.
Mwalimu huyo aliacha maagizo ya kuzikwa siku ya wapendanao ya Valentino na ex wake huyo kuhusika katika kuisoma eulogy ya mazishi yake.