logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bosi wa zamani wa polisi, Kingori Mwangi amefariki

Marehemu King'ori Mwangi alifanyiwa upasuaji kwenye tumbo lake ambalo lilidhoofika, rafiki wa familia alisema.

image
na Samuel Maina

Habari11 February 2024 - 07:18

Muhtasari


  • •Marehemu King'ori Mwangi alifanyiwa upasuaji kwenye tumbo lake ambalo lilidhoofika, rafiki wa familia alisema.

Aliyekuwa mkuu wa polisi Zachary Kingori Mwangi amefariki.

Kingori alifariki Jumapili, Februari 11 katika hospitali moja jijini Nairobi alikokuwa amelazwa.

Familia yake ilituma ujumbe kwa marafiki zake kutangaza kifo chake.

“Tungependa kufahamisha umma kuhusu kifo cha Bw Kingori Mwangi, afisa wa polisi aliyestaafu. Kingori amefariki leo asubuhi katika hospitali ya Nairobi alikokuwa akipokea matibabu. Familia itasasisha umma kuhusu mipango ya mazishi. Familia ya Kingori Mwangi,” ulisomeka ujumbe huo.

Alifanyiwa upasuaji kwenye tumbo lake ambalo lilidhoofika, rafiki wa familia alisema.

Kingori aliwahi kuwa Afisa wa Polisi wa Mkoa katika mikoa ya Nairobi, Mombasa na Magharibi.

Pia aliwahi kuwa mkurugenzi wa operesheni katika makao makuu ya polisi, msemaji wa polisi, mkurugenzi wa Kampasi ya Polisi ya Kenya iliyoko Kiganjo na msaidizi mkuu wa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kenya.

Wenzake wa zamani walimsifu kama mtu aliyejitolea ambaye alikuwa thabiti kila wakati katika kazi yake.

"Alikuwa mtu mzuri. Apumzike kwa amani,” afisa mmoja mkuu alisema.

Bw King'ori alistaafu kutoka kwa huduma hiyo mnamo 2021 baada ya kufikia umri wake wa kustaafu


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved