Mwanamke aliyekuwa pamoja na Kiptum wakati wa ajali aruhusiwa kutoka hospitali

Wengine ambao walikua kwa ajali hiyo ni Kelvin Kiptum na kocha wake, Gervis Hakizimana.

Muhtasari
  • Kulingana na ripoti za polisis, Kelvin Kiptum alikua akiendesha gari lake aina ya Toyota Premio alipopoteza mwelekeo na kutua kwenye shimo.
  • Sharon Chepkirui Kosgei alikimbizwa hospitali ya Moi Teaching and Referral na majeraha makubwa kufuatia ajali hiyo
amefariki akiwa na umri wa miaka 24.
Kelvin Kiptum amefariki akiwa na umri wa miaka 24.
Image: HISANI

Abiria wa kike ambaye alikuwa pamoja na bingwa wa marathon Kelvin Kiptum wakati wa ajali, ameruhusiwa kutoka hospitalini kuenda nyumbani.

Sharon Chepkirui Kosgei alikimbizwa hospitali ya Moi Teaching and Referral na majeraha makubwa kufuatia ajali hiyo iliyofanyika kwenye barabara ya Eldoret-Kiptagat.

Mwingine ambaye alikuwepo wakati wa ajali hiyo ni Kelvin Kiptum na kocha wake, Gervis Hakizimana ambaye pia aliaga.

Kulingana na ripoti za polisi, Kelvin Kiptum alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Premio alipopoteza mwelekeo na kutua kwenye shimo.

Aliendelea kuendesha ndani ya shimo kwa takriban mita 60 kabla ya kugonga mti mkubwa. Matokeo ya ajali hiyo yalikuwa Kelvin na kocha wake kukufa hapo hapo.

Mwili wa Kiptum na Hakizimana  ulipelekwa chumba cha maiti wa  Racecourse Eldoret kwa uchunguzi.

Kiptum alipanda cheo wakati alipata bingwa wa marathon ambayo ilifanyika Valencia mwaka wa 2022.

Aliendelea kupanda mwaka wa 2023 aliposhinda London marathon na rekodi ya 2:01:25. 

Ilikuwa hata hivyo mwezi wa Okotoba, Kiptum alikuwa katika vichwa vya habari baada ya kuvunja rekodi kwa kutumia saa 2:00:35. Alikuwa mwanaume wa kwanza kukimbia marathon chini ya masaa mawili na dakika moja.