Uvumi waibuka kuwa Hassan Mugambi na Chumutai Goin wamepata kazi serikalini

Mwanahabari Chemutai Goin pia inadaiwa ataondoka mwezi Machi kujiunga na ofisi ya Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang'ula.

Muhtasari
  • Mugambi baada ya kuhama runinga ya K24 alijiunga Citizen TV mwaka wa 2016  Septemba kama ripota wa Kiswahili. 

  • Chemutai Goin pia alituzwa na rais katika sherehe za Madaraka  mwaka wa 2020.
Hassan Mugambi na Chemutai Goin
Image: Instagram

Wanasema penye moshi hapakosi moto, uvumi umezuka mitandaoni kuwa mwanahabari tajika Hassan Mugambi huenda yuko njiani kuondoka Citizen TV.

Kulingana na duru karibu na mwanahabari huyo, anapanga kuondoka Citizen mwezi Machi kwenda kufanya kazi katika afisi ya waziri wa Ulinzi, Aden Duale.

Mwanahabari mwenzake Chemutai Goin pia inadaiwa ataondoka mwezi Machi kujiunga na ofisi ya Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang'ula.

Uvumi huu umezua mjadala mtandaoni wengine wakisema kuwa wata'miss wanahabari hao, huku wengine wakisema kuwa serikali inachukua wanahabari wote wazuri kama Hussein Mohammed na Kanze Dena.

Mugambi baada ya kuhama runinga ya K24 alijiunga Citizen TV mwaka wa 2016  Septemba kama ripota wa Kiswahili. 

Chemutai Goin alifanya kazi kwa radio kabla ya kuenda runinga kama ripota wa siasa. 

Chemutai Goin pia alituzwa na rais katika sherehe za Madaraka  mwaka wa 2020.