Johansen Oduor azungumzia safari yake ya upatholojia

" Sikuwa nataka kufanya postmortem kwa sababu kuna ubaguzi mwingi na watu wanatuogopa, " alisema.

Muhtasari
  • Johansen Oduor alifichuwa kuwa alikuwa na nia ya kutafuta kazi katika uwanja wa matibabu lakini hakuwa na nia ya postmortem.

  • Alifichua kuwa yeye anapenda muziki sana hivyo wakati hafanyi upasuaji, anaskia muziki na pia anatalanta ya kuimba.
Mwanapotholojia Johansen Oduor
Image: COLLINS APUDO

Mwanapatholojia mkuu wa serikali, Johansen Oduor alifichuwa kuwa alikuwa na nia ya kutafuta kazi katika uwanja wa matibabu lakini hakuwa na nia ya postmortem kwa sababu kuna ubaguzi kutoka kwa watu ambao wanaowagopa wataalamu kama hao.

" Sikuwa nataka kufanya postmortem kwa sababu kuna ubaguzi mwingi na watu wanatuogopa".

Aliendelea kueleza kuwa aliambia babake kuwa alikuwa anataka kukuwa daktari ili asaidie jamii lakini babake alishangaa kwa sababu alikuwa anataka akue mwalimu.

Katika mahojiano na Fridah Mwaka siku ya jumamosi, mwanapatholojia huyo alieleza kuwa wakati alimaliza chuo kikuu na kuhitimu, wizara ya afya ilimuweka katika Chumba cha kuhifadhia maiti cha City

" Wizara ya afya baada ya kumaliza chuo kikuu iliniweka Chumba cha kuhifadhia maiti cha City. Hata ilikuwa mara yangu ya kwanza kuenda huko na nilikuwa na uwoga mwingi sana. Lakini niliangalia hao maiti na  ni watu wametoka Kibera na Mathare mali nilitoka. Nikasema sasa nikitoroka hawa watasaidiwa na nani". Oduor alieza.

Aliendelea kusema kuwa kazi ya upathologia iko na mabishano mengi na watu kunyosheana vidole hivyo alikuwa  anawaza kama atawezana nayo lakini akakumbuka alikuwa ameamua kuwa anataka kusaidia jamii kwanza ambao  wanatoka katika umaskini.

Alifichua kuwa yeye anapenda muziki sana hivyo wakati hafanyi upasuaji, anaskia muziki na pia ana talanta ya kuimba.

" Mimi napenda muziki sana na pia naweza imba. Wakati nilikuwa chuo kikuu nilikuwa nilikuwa narap katika mashindano." Napenda pia kutazama sinema sana. Hakuna Sinema mpya amabyo inaweza tokea na nisiitazame".

Alifichua kuwa ako na familia. Watoto watatu na wa kwanza ako na miaka 21.

Alimpa kongole babake kwa kuwa alimwaminia sana hata wakati alikuw amepoteza matumaini, baba yake alikuwepo kila mara kumtia moyo.

Mama yake pia na maprofessa wake walimsaidia katika safari yake. 

Wakati wa mahojiano hiyo alifichuwa kuwa alizaliwa mwaka wa 1974 na kukulia ndani Mathare baadaye alienda Chuoo kikuu ya Nairobi ambapo alitunukiwa shahada ya kwanza ya sayansi ya dawa na upasuaji. Baadaye alifanya masters katika patholojia.