Mke wa Kelvin Kiptum, Bi Asenath Rotich amesifu bwanake yake katika ujumbe alioandikia marehemu.
Wakati akisoma alichoandika, alitokwa na machozi huku mwanamke mwingine akimfariji. Alieleza vile atamiss kampani ya mume wake.
"Mpenzi wangu mpendwa, siwezi kujifunza jinsi ya kusema kwaheri kwako Kwa vidole dhaifu na maumivu moyoni mwangu Ni ajabu kwamba leo nimejifunza kukaa na watoto wetu wapendwa bila wewe kurudi nyumbani tena", alisema.
Pia aliapa kuwatunza watoto wao wawili wadogo.
"Ninaahidi kukusanya nguvu zangu kwa ajili ya watoto wetu. Ninatumaini kwamba ulimwengu wa roho utanitia moyo kusimama kama nguzo kwa watoto wetu. Ninaahidi kuwafanya watabasamu kwa heshima yako".
Huku akiomboleza Kiptum kama kipenzi cha roho yake, Bi Rotich alisema " Nimelia hadi hakuna tena, nitakukosa na upendo wangu kwako milele. Mpaka tukutane tena".
Alisema Kiptum alikuwa Mume mzuri ambaye maisha yake ambaye maisha yake yalikatizwa wakati ambapo nyota yake ilikuwa inang'aa.
"Wakati nyota yako ilipokua kuwa angavu zaidi, Mungu alikuchagua. Umekuwa baba bora kwa watoto wetu; nitamiss kampuni yako.Tukutane tena. Bye" Rotich aliandika.
Viongozi wengi akiwemo Rais William Ruto wanahudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa katika uwanja wa ASK Chepkorio huko Elgeiyo Marakwet.
Kiptum atazikwa katika nyumba yake mpya huko Naiberi, Uasin Gishu.