Moto mkubwa uliozuka katika jengo la ghorofa katika mji mkuu wa Bangladesh Dhaka umeua takriban watu 46 na kujeruhi makumi ya wengine.
Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, moto huo ulianza katika mgahawa katika eneo la orofa saba mwendo wa saa 22:00 kwa saa za huko (16:00 GMT) siku ya Alhamisi.
Watu sabini na watano waliokolewa na kadhaa kupelekwa hospitalini.
Moto huo ulidhibitiwa baada ya saa mbili.
Chanzo cha moto huo kinachunguzwa, zima moto walilaumiwa kuwa usalama ulidorora.
Afisa wa zimamoto alisema jengo hilo halikuwa na njia ya dharura ya kutokea na mitungi ya gesi ya kupikia iliwekwa kwenye ngazi na kwenye majiko ya migahawa.
Waziri wa Afya Samanta Lal Sen alisema kuwa takriban watu 33, wakiwemo wanawake na watoto, wametangazwa kufariki katika Hospitali ya Chuo cha Dhaka.
Takribani wengine 10 walifariki katika hospitali kuu ya mji huo.
22 walikuwa katika hali mbaya, Bw Sen alisema.
Huduma za dharura ziliitwa kwenye mgahawa wa Kacchi Bhai katika jengo la ghorofa saba, kulingana na gazeti la Daily Bangladesh.
Jumba ambalo jengo liko pia lina migahawa mingine, pamoja na maduka kadhaa ya nguo na simu za mkononi.