logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Magavana wenye kaunti zenye visa vingi vya mimba za utotoni wapewa kadi nyekundu

KHRC ilitoa ripoti Alhamisi kwamba kaunti 10 zinaongoza katika visa vya mimba za utotoni

image
na Davis Ojiambo

Habari08 March 2024 - 05:24

Muhtasari


  • • Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa visa 452 huku Kakamega ikiwa ya pili kwa visa 328, Bungoma visa 294, Nakuru visa 283.
KHRC yatoa kadi nyekundu kwa kaunti zenye visa vingi vya mimba za utotoni

Magavana wa kaunti kumi pamoja na waziri wa afya Susan Nakhumincha wameonyeshwa kadi nyekundu ya tume ya kutetea haki za kibinadamu KHRC kutokana na ongezeko la visa vya mimba za utotoni katika kaunti na idara zao.

KHRC ilitoa ripoti Alhamisi kwamba kaunti 10 zinaongoza katika visa vya mimba za utotoni, Nairobi ikiwa kileleni huku nafasi ya kumi ikiwa inashikiliwa na kaunti ya Narok.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa visa 452 huku Kakamega ikiwa ya pili kwa visa 328, Bungoma visa 294, Nakuru visa 283.

Kaunti zingine ambazo magavana wao walipewa kadi nyekundu na KKHRC ni pamoja na Kilifi yenye visa 224, Meru visa 206, Kisii visa 192, Machakos visa 178 na Narok visa 176.

KHRC pia imemkashifu Katibu wa waziri wa Afya Susan Nakhumicha kwa kile wanachodai kushindwa kuchukua hatua zinazoonekana na za kimaendeleo kushughulikia tatizo la mimba za utotoni.

“Tumetoa kadi nyekundu kwa Nairobi, Johnson Sakaja (Kakamega), Kenneth Lusaka (Bungoma), Fernades Barasa (Kakamega), Susan Kihika (Nakuru), Waving Ndeti Machakos, Kimani Wamatangi (Kiambu), Gideon Mung’aro (Kilifi), Kawira Mwangaza (Meru), Simba Arati (Kisii) na Patrick Ole Ntutu wa Narok,” Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa KHRC Davis Malombe alisema.

Kulingana na Utafiti wa Demografia na Afya nchini Kenya wa 2022, kaunti hizo 20 zilikuwa na idadi kubwa zaidi ya mimba zilizoripotiwa miongoni mwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 10 na 19.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved