logo

NOW ON AIR

Listen in Live

{Picha} Jinsi kongamano la Siku ya Wanawake lililoandaliwa na Radio Africa Events lilivyokuwa

Kongamano hilo lilianza saa moja asubuhi na kumalizika mwendo wa saa sita mchana.

image
na Samuel Maina

Habari08 March 2024 - 12:58

Muhtasari


  • • Radio Africa Events iliangazia maeneo muhimu ambapo kuwekeza kwa wanawake kuna jukumu muhimu katika kuharakisha maendeleo.
  • •Kongamano hilo lilianza saa moja asubuhi na kumalizika mwendo wa saa sita mchana.

Siku ya Ijumaa, Machi 8, kampuni ya vyombo vya habari ya Radio Africa Group kupitia Radio Africa Events iliwakaribisha wanawake kutoka matabaka mbalimbali katika Capital Club kwa ajili ya kongamano maalum la wanawake kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Hafla hiyo iliyopewa jina la "Banking on the Future of Women" ililenga kuwapa wanawake zana, rasilimali na fursa za kuimarisha uwezeshaji wao kiuchumi.

Katika hafla ya mwaka huu, Radio Africa Events iliangazia maeneo muhimu ambapo kuwekeza kwa wanawake kuna jukumu muhimu katika kuharakisha maendeleo.

Waliohudhuria ni pamoja na Dkt Lucy Mathenge, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya utawala katika UN Women-Kenya, Sera Kitusya, Mkurugenzi Mtendaji wa Belva Group, Anita Chege ambaye ni GM wa uvumbuzi HF, Zuhura Ogeda Odhiambo ambaye ni mwenyekiti wa MSK na Mfadhili. katika MRSA, Imelda Ngunzu, mkurugenzi wa ushirikiano wa kimataifa na sehemu za uvumbuzi Mastercard.

Kiprono Kittony ambaye ni Mwenyekiti wa Soko la Hisa la Nairobi na mwanzilishi wa Radio Africa Group na Mkurugenzi Mtendaji Patrick Quarcoo pia walihudhuria.

Kongamano hilo lilianza saa moja asubuhi na kumalizika mwendo wa saa sita mchana.

Tazama baadhi ya picha za hafla hiyo:-


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved