logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uuzaji wa nyama wapigwa marufuku mjini Kampala

Mamlaka ya wanyama nchini Uganda imeripotiwa kupiga marufuku uuzaji wa nyama katika mji mkuu, Kampala.

image
na Samuel Maina

Habari09 March 2024 - 06:51

Muhtasari


  • •Mamlaka ya wanyama nchini Uganda imeripotiwa kupiga marufuku uuzaji wa nyama katika mji mkuu, Kampala.

Mamlaka ya wanyama nchini Uganda imeripotiwa kupiga marufuku uuzaji wa nyama katika mji mkuu, Kampala, kama sehemu ya vikwazo vya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta, unaoathiri wanyama.

"Usafirishaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe na bidhaa zitokanazo na nyama zao, kupitia au ndani ya Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala, Wilaya ya Kampala, ni marufuku hadi itakapotangazwa tena," Wizara ya Kilimo, Sekta ya Wanyama na Uvuvi ilisema katika barua iliyotajwa na vyombo vya habari kadhaa vya ndani.

"Masoko ya mifugo, sehemu za vichinjio, ikiwemo kunakouzwa nyama, viwanja vya kupakia na maonyesho ya wanyama katika wilaya nzima yanafungwa mara moja."

Barua hiyo ni ya tarehe 1 Machi lakini ilipokelewa na mamlaka ya Kampala siku ya Alhamisi, kulingana na ripoti za gazeti la kibinafsi la Daily Monitor.

Afisa mmoja wa jiji aliliambia gazeti hili kwamba watafanya kazi na mashirika mengine kutekeleza hatua za karantini, lakini vyombo vya habari vya ndani vinasema sehemu za kuuza nyama za jijini bado zinaendesha shughuli zake.

Ugonjwa unaoambukiza sana wa mguu na mdomo husababisha homa na malengelenge yenye uchungu ndani ya mdomo na chini ya kwato - na unaweza kusababisha kifo kwa wanyama wadogo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved