KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 12.
Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Uasin Gishu, Homa Bay, na Kwale.
Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu katika mtaa wa Karen zitakosa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa katika maeneo ya Tigoni na Kabuku katika kaunti ya Kiambu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Ngecheck na Ngeria katika kaunti ya Uasin Gishu pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Rapora, Mirunda na Lwanda katika kaunti ya Homa Bay zitakuwa bila stima.
Katika kaunti ya Kwale, baadhi ya sehemu za eneo la Galu zitaathirika na kukatizwa kwa stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.