logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanahabari Rita Tinina alipatikana amekufa ndani ya nyumba yake

Alipaswa kuwa zamu katika NTV ambako alifanya kazi lakini alishindwa kuripoti.

image
na Davis Ojiambo

Habari17 March 2024 - 13:08

Muhtasari


  • • Alipaswa kuwa zamu katika NTV ambako alifanya kazi lakini alishindwa kuripoti.
RITA TININA

Mwanahabari mkongwe Rita Tinina amefariki dunia. Polisi walisema mwili wa Tinina ulipatikana katika nyumba yake ya Kileleshwa jijini Nairobi Jumapili, Machi 17.

Alipaswa kuwa zamu katika NTV ambako alifanya kazi lakini alishindwa kuripoti.

Hilo lilifanya wasimamizi wa kazi yake waende kwenye nyumba ambayo mwili huo ulipatikana.

Chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana, polisi walisema. Familia yake ilikuwepo polisi walipofika kuuchukua mwili huo hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Alikuwa ni mama wa msichana mmoja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved