logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kumkumbuka Magufuli:Saa 24 za mwisho za aliyekuwa rais wa Tanzania, aliyopitia Samia kabla ya kuapishwa

Alikuwa rais wa kwanza nchini Tanzania kufariki dunia akiwa madarakani.

image
na Samuel Maina

Habari18 March 2024 - 04:46

Muhtasari


    "Kitu ambacho sijawahi kusema ni kuwa Rais (John Magufuli) aliniita akaniambia CDF njoo, akaniambia siwezi kupona. Waamuru hao madaktari wanirudishe nyumbani. Nikamwambia mheshima sina hayo mamlaka. Akasema CDF huwezi kuwaamuru wanirudishe nyumbani? Nikamwambia suala la afya si la CDF," Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Venance Mabeyo anasimulia na kueleza kuwa alimshauri kuwa madaktari walikuwa wanaendelea vyema kumpambania.

    Tareha 17 machi ilikua kumbukumbu ya miaka mitatu tangu kufariki kwa Rais John Magufuli.

    Rais wa kwanza nchini Tanzania kufariki dunia akiwa madarakani.

    Katika mahojiano yaliyofanywa na Daily News Digital, kiongozi huyo mkuu wa majeshi mstaafu alielezea hali ilivyokuwa saa 24 kabla ya Rais Magufuli kufariki lakini pia saa 40 za Rais wa sasa, Samia Suluhu kabla ya kuapishwa.

    Mabeyo ambaye alihudumu kama Mkuu wa Majeshi (CDF) tangu 2017 hadi 2022 anasema wakati Rais anaugua yeye na wenzake wawili kama viongozi wa ulinzi na usalama tulishirikishwa.

    Anasema, "Kujua hali yake ilivyo, tulienda kila asubuhi na jioni kumuona. Tulikuwa na nafasi yetu kama wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama tunashauriana…

    "Badae tukampeleke Hospitali ya Mzena, pale kulikuwa na utulivu na tukaweka usalama pale na madaktari walipelekwa kumwangalia kwa wakati wote," anaeleza

    SAA 24 Kabla kufariki

    Mabeyo anasimulia kuwa siku moja kabla ya kifo cha Rais Magufuli, hali ilibadilika na yeye alitambua hali imebadilika.

    Anasema, "Aliona hali yake na Mwenyenzi Mungu alimuonesha kuwa hata pona na alichosema nirudisheni nyumbani nikafie nyumbani tukamwambia hapa uko mikono salama."

    Alitaka maombi

    Baada ya kuona CDF ana msimamo wa kutoamrisha arudi nyumbani, akamwambia amuitie paroko wake wa Kikatoliki, paroko wa St Peters anaitwa Askofu Makubi na Kadinali Pengo.

    "Hiyo asubuhi tulimtafuta Kadinali Pengo lakini alikuwa ibadani. Baada ya muda akaniuliza haujampata Pengo, nikamwambia alikuwa kwenye ibada ila nimeshamtumia usafiri na atafika...

    "...waliwasili na kumsalia kwa taratibu za kikatoliki. Walifanya ibada na kumpa sakramenti ya upako wa magonjwa kwa anayekuwa katika hatari ya kufariki. Alipumizka na ilipofika mchana saa nane, walitupigia na kutueleza hali ya Rais si nzuri. Tulimkuta na hakuweza kuongea," anaeleza.

    Alifariki saa 12 unusu jioni

    Kiongozi huyo alisema Rais Magufuli aliendelea kupata tiba mpaka jioni. "Ilipofika saa 12 na nusu au saa moja kasoro akakata roho. Tulikuwa wakuu wa vyombo watatu, pale nilikuwa mimi, IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) na DGIS .

    Taafira ya kwanza iende kwa nani?

    Anasema, "Makamu wa Rais, Samia wakati huo alikuwa Tanga, Waziri Mkuu hakuwa Dar, alikuwa Dodoma, katibu mkuu Kiongozi naye alikuwa Dodoma. Tulikuwa sisi watatu tu"

    Mabeyo anasema walimpa taarifa Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi kutakiwa Dar na walipofika aliwaeleza kuwa Rais amefariki.

    "Tukaanza kushauri tunafanyaje, nani atangaze hizi Habari kwenye vvyombo vya habari ili wananchi wafahamu. Tukaanza kutafuta katiba inasema nini. Mtu pekee anaweza kutangaza ni Makamu wa Rais. Tukasema yuko Tanga tarifa zinamfikiaje? Tukafanya utaratibu," alisema na kuongeza kuwa walitoa taarifa kwa Familia ya Magufuli kisha ilipofika saa 5 usiku ndipo ilipotangazwa kwa umma kuwa amefariki.

    Uapisho wa Samia ulichelewa

    Mabeyo anasema kulikuwa na mawazo kinzani mawili, Samia aapishwe kuwa Rais kabla ya maziko au baada ya mazikoo.

    "Nako kukawa na mjadala. Tukajiuliza kuna Marais wengine watakuja kumzika mwenzao, tukasema atapokelewa na makamu wa Rais lakini lazima kuwe Rais? Basu tukafikia maamuzi kwamba makamu wa Rais aapishwe kama Rais. Na ndio maana ilipita siku mbili, lakini kikatiba haitakiwa, alipaswa kuapishwa ndani ya saa 24, atangazwe kuwa Rais," alieleza Mkuu huyo.

    Baadhi walipinga sherehe za uapisho wa Samia

    Tarehe 17, 18 zikapita na 19 ndipo alipoapishwa ila kwa mujibu wa Mabeyo kulikuwa na majadiliano ya namna ya kumuapisha.

    " Tunamuapishaje? wengine wakasema kusifanyike sherehe, wengine wanasema ifanyike.Sasa Mimi kama mkuu wa majeshi nilisema paredi lazima iwepo, bendera ya Amiri Jeshi Mkuu lazima ipande kwa gwaride...

    "...nikasema huyu ni Amiri Jeshi Mkuu anaapishwa asipoapishwa kwa taratibu hizo za kitaifa, jeshi halitamtambua," anaeleza.

    Mjadala mpya Samia asiitwe amiri jeshi mkuu

    "Sisi tuliwaambia watu jeshini hatuna wanawake. Yaani hatutambui watu kama mwanaume au mwanamke. Ndio maana jeshini tuna afisa na askari hivyo Samia ni

    Amiri jeshi na si amirati...

    "...mjadala ulivyozidi tukawauliza Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) Amirati maana yake nini, wakaeleza vizuri, tukasema tuendelee hapa, anasema na kueleza kuwa Amirati ni cheo kwa nchi za kifalme zinazotawaliwa kidini.


    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved