logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Facebook na Instagram kuanza kulipa wabunifu wa Kenya kuanzia Juni

Facebook na Instagram zitaanza kuwalipa waundaji Maudhui kuanzia mwezi wa Juni.

image
na Davis Ojiambo

Habari19 March 2024 - 09:23

Muhtasari


  • Waundaji wa maudhui nchini Kenya watapata pesa kwa kuchapisha kwenye mitandao ya Facebook na Instagram kuanzia Juni mwaka huu kufuatia makubaliano kati ya rais wa masuala ya kimataifa Nick Clegg.
Meta yaeleza kilichosababisha hitilafu kwenye Facebok, Instagram

Wabunifu wa maudhui nchini Kenya watapata pesa kwa kuchapisha kwenye mitandao ya Facebook na Instagram kuanzia Juni mwaka huu kufuatia makubaliano kati ya rais  William Ruto na kiongozi wa Meta Nick Clegg.

Katika mkutano kwenye Ikulu ya Nairobi, idara ya rais mawasiliano ya rais  makubaliana hayo ni kilele cha jitihada za mwaka mzima za serikali kuwa na wabunifu wa kupata mapato kutokana na maudhui yao ya mtandaoni kama wanavyofanya kwenye majukwaa mengine kama vile Youtube na X(Twitter)

"Watayarishi wa maudhui wa Kenya wanaokidhi vigezo vya kustahiki sasa watapata mapato kutokana na nafasi zao za facebook na Instagram tunapoanza uchumaji wa mapato kufikia Juni mwaka huu", alisema Bw. Clegg.

Rais william Ruto alipongeza hatua hiyo, akibainisha kuwa itafungua fursa mpya za kuwaingizia kipato vijana wa Kenya, huku akitoa wito kwa meta kuunganisha malipo kwa M-pesa.

"Sasa waundaji wa maudhui wanaweza kuanza kuchuma mapato kutokana na mawazo na ubunifu wao. Tunatumia nafasi ya kidijitali kuunda nafasi za kazi kwa mamilioni ya vijana wasio na kazi katika nchi yetu", Ruto alisema.

Ili kuhitimu kwa programu, mtayarishaji anahitajika kuwa na angalau wafuasi 5,000 kwenye wasifu wake wa kibinafsi wa Facebook au wafuasi 10,000 kwenye ukurasa wa Facebook na angalau video 5 za moja kwa moja kwenye wasifu au 3 kwenye ukurasa.

Maudhui ya video yaliyotumwa kwenye wasifu wa Facebook lazima yawe na angalau dakika 60,000 zilizotazamwa katika siku 60 zilizopita kutoka kwa wafuasi wa kikaboni huku , kwa ukurasa, hitaji ni dakika 600,000 kutazamwa ndani ya muda sawa.

Kwa wadadisi wa sekta, Facebook huwalipa waundaji maudhui ksh. 1,074 (dola 8) hadi ksh. 2,685 (dola 20) kwa kila mwonekano 1,000 na wastani wa Gharama kwa Maili katika nchi nyingi za Afrika huanzia chini ya ksh. 1,074 hadi 1,342 (dola 10) kwa sababu sekta ya masoko haijaendelezwa ikilinganishwa na nchi kama Marekani, Australia, Kanada na Uingereza.

Haya yanajiri wakati data mpya kutoka kwa Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya zinaonyesha kuwa Facebook imeshinda mfumo wa utumaji ujumbe wa papo hapo wa Whatsapp na kuwa programu inayotumika zaidi ya mitandao ya kijamii nchini, ikiashiria uwezo mkubwa wa kupata mapato kwa watayarishi mara tu kipengele cha uchumaji mapato kitakapoanza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved