Mwanamke wa Ohio nchini Marekani ambaye alienda likizo ya siku 10 ya kujivinjari huku akiwa amemuacha nyumbani mwanawe wa kike mwenye umri wa miezi 16 akifa kwa njaa ameamriwa kukaa gerezani maisha yake yote.
Kwa mujibu wa kesi hiyo iliyofuatiliwa na USA Today, Kristel Candelario, 32, alipokea hukumu yake Jumatatu katika mahakama ya serikali huko Cleveland baada ya kukiri shtaka moja la mauaji ya kuzidisha na kuhatarisha mtoto katika kifo cha binti yake Jailyn.
Hakimu aliyesimamia kesi ya Candelario, alisema kusafiri nje ya jimbo huku akiacha nyumba ya mtoto peke yake bila chakula ni "usaliti wa mwisho" ambao unastahili adhabu kali zaidi ya kisheria inayopatikana.
"Kama vile hukumruhusu Jailyn kutoka katika makali ya njaa, vivyo hivyo unapaswa kutumia maisha yako yote kwenye seli bila uhuru," hakimu alisema wakati wa kusikilizwa kwa hukumu ya Candelario.
"Tofauti pekee itakuwa [kwamba] jela angalau itakulisha na kukupa kioevu ambacho ulimnyima."
Candelario, wakati huohuo, alimwambia Sheehan kwamba alisali kila siku kwa ajili ya msamaha.
"Kuna maumivu mengi ambayo ninayo kuhusiana na kufiwa na mtoto wangu, Jailyn," alisema Candelario, ambaye inasemekana ametatizika na unyogovu na matatizo yanayohusiana na afya ya akili.
"Nimeumia sana kwa kila kitu kilichotokea. Sijaribu kuhalalisha matendo yangu, lakini hakuna aliyejua jinsi nilivyokuwa nikiteseka na kile nilichokuwa nikipitia.”
Bila kueleza zaidi, Candelario alimalizia hivi: “Mungu na binti yangu wamenisamehe.”
Kwa mujibu wa USA Today, Waendesha mashtaka walimshtaki Candelario kwa kwenda likizoni Detroit na Puerto Rico kuanzia tarehe 6 Juni huku wakimuacha Jailyn nyuma kwenye uwanja wa michezo nyumbani kwao ukingoni mwa kitongoji cha Cleveland West Boulevard.
Siku chache za safari, gazeti la New York Post liliripoti, Candelario alienda kwenye mtandao wa kijamii na kuweka picha yake akitabasamu, bila viatu na akiwa amevalia suti ya kuoga ufukweni. Maelezo ya picha hiyo yalisomeka: "Wakati unaofurahiwa ni wakati wa kweli ulioishi."
Candelario hakurudi nyumbani hadi karibu 8am mnamo 16 Juni. Alimkuta Jailyn akiwa hapunui kisha akapiga simu 911. Wahudumu wa dharura walifika, waliamua kwamba Jailyn alikuwa "amepungukiwa na maji sana" na muda mfupi baadaye wakatangaza kifo chake.
Baada ya uchunguzi wa maiti, ofisi ya mchunguzi wa eneo hilo iliamua kwamba Jailyn alikufa kwa njaa na upungufu mkubwa wa maji mwilini. Mamlaka zilimshtaki Candelario kwa mauaji, huku waendesha mashtaka wakionyesha kuwa walikuwa na haki ya kutekeleza hukumu ya kifo dhidi yake.
Candelario alikiri hatia tarehe 22 Februari kama sehemu ya makubaliano ambayo yalimwacha akikabiliwa na kifungo cha maisha jela bila msamaha. Waendesha mashtaka pia walikubali kufuta shtaka linalohusiana na shambulio la jinai.
Katika hukumu ya Jumatatu, hakimu alimpa Candelario adhabu kali zaidi inayoweza kupatikana kwake baada ya kujibu ombi lake la hatia.
Katika taarifa baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, mwendesha mashtaka wa Cleveland Michael O'Malley alisema Candelario alionyesha "ubinafsi usiofikirika" katika kumuua Jailyn.