Ni mambo na vitendo ambavyo akina babu zetu wakiamka kutoka kaburini watashangaa, jinsi vizazi vyao wanafanya na kujitosa kwenye mambo bila ya kujali kesho yao.
Tumekuwa tukiyaona kwa televisheni na hata filamu bila ya kujua kuwa ni mambo ambayo yanatendeka kwenye familia zetu.
Wanandoa wa siku hizi hawajali kuhusu maadili ya ndoa zao wanaona tu ni filamu au mchezo wa kuigiza wanafanya.
Nikiwa kwenye pilkapilka zangu nilipatana na mwanada mmoja ambaye alimwaya mtama mchana peupe kwa kusimulia jinsi alivyokuwa na hisia za kimapenzi na baba mkwe wake.
Kulingana na mwanadada huyo alifanya tendo la ndoa na baba mkwe wake siku moja kabla ya harusi yake.
Aidha alisema kuwa hakua tu na hisia za kimapenzi kwa baba mkwe siku hiyo bali alianza kumpenda punde tu alipotambulishwa na mumewe kwa wazazi wake.
Mwanadada huyo alisema kuwa ni siri ambayo mume wake hajawahijua kwa miaka 8 ambayo wamekuwa pamoja.
Huu hapa usimulizi wake;
"Nimekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na baba mkwe wangu kwa miaka kadhaa sasa, ndio namuona kama baba mkwe lakini linapokuja upande wa kimapenzi ananitimizia mahitaji yanhu kuliko mwanawe yaani mume wangu
Ni siri ambayo nimehishi nayo na mabyo nataka kumwambia mume wangu lakini naogopa kwani nitaleta chuki na ugomvi kati ya mume wangu na baba yake mzazi,cha kushangaza ni kuwa nilifanya tendo la ndoa naye siku moja kabla ya harusi yangu na sina majuto na jambo ambalo nilifanya na uhusiano ambao tumekuwa nao kwa muda sasa.
Sijui nimtobolee mume wangu siri hii, kwani inanisumbua akili, nina uhakika kuwa mume wangu amekuwa mwaminifu kwangu, nilimshauri baba tukomeshe tabia hii lakini hataki kunisikia wala kusikia lolote kuhusu kumaliza uhusiano wetu nisaidieni nifanye aje."
Je unaweza kumsaidia vipi mwanadada huyu ambaye yiuko kwenye nia panda?