logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa stima Jumatano -KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano. Machi 27.

image
na Samuel Maina

Habari27 March 2024 - 04:08

Muhtasari


  • •KPLC imetangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti nne yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano. Machi 27.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Tharaka Nithi, Kiambu na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za barabara ya Waiyaki na ya Raphta zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Kianjagi na afisi za kaunti za Chogoria katika kaunti ya Tharaka Nithi zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Toll Station na Murera Coffee katika kaunti ya Kiambu yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Watamu katika kaunti ya Kilifi zitaathirika na kukatizwa na umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved