Ujio wa utandawazi umeona biashara za vitu mbalimbali zikifanyika mitandani, ikiwemo biashara ya kubadilisha sarafu za kidijitali hufanyika.
Lakini ujio wa biashara hii pia umekuwa ukiibua maswali mbalimbali, haswa kuhusu usalama wad eta za kibinafsi za watu wanaojiunga na mitandao ya kushiriki kaitka biashara ya sarafu, kwa kimombo cryptocurrency.
Hili limefanya serikali nyingi kufungua nyuzi zao na baadhi ya mataifa kupiga marufuku au kusitisha shughuli za baadhi ya kampuni za cryptocurrency kwenye mataifa yao.
Hizi hapa ni baadhi ya kampuni za cryptocurrency na mataifa ambayo zimefungiwa kuhudumu.
Kampuni ya Worldcoin ambayo ilianzishwa mwaka jana na mwanzilishi wa Open AI, Sam Altman imekuwa ikipata pigo baada ya kupokea nyaraka za kutakiwa kusitisha shughuli zake katika mataifa mbali mbali.
Worldcoin
Mwezi Agosti ilipata pigo nchini Kenya baada ya mamlaka kuifungia kwa kile walisema ni wasiwasi juu ya ulinzi wa deta za kibinafsi za watu, katika jukwaa lao la kufanyia mboni za watu scanning kama njia moja ya kuchukua maelezo yao ya kibinafsi.
Wiki tatu zilizopita, taifa la Uhispania lilikuwa la pili kuifungia Worldcoin kuedneleza huduma zao katika taifa hilo la Ulaya kwa sababu sawia na hizo.
Na sasa Jumanne, mamlaka nchini Ureno pia zilisitisha operesheni za Worldcoin kaitka taifa hilo, wakitilia wasiwasi wao kuhusu ulinzi wa maelezo ya kibinafsi ya watu haswa katika suala zima la kumlika mboni za macho.
Binance
Hii ni sarafu nyingine iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani, haswa baada ya kufanikiwa kumpata mwanasoka Cristiano Ronaldo kama balozi wao wa masoko.
Licha ya umaarufu wao, Binance pia wamekuwa wakikumbwa na matatizo mbaimbali la hivi karibuni liiwa ni kujiondoa katika soko la Nigeria na kuiondoa Naira – sarafu ya taifa hilo – kwenye soko lake.
Binance pia walikuwa wamekabiliwa na vikwazo kadhaa vya ufikiaji kutoka kwa mamlaka nyingi kama vile Uingereza, Singapore na Kanada.
Taarifa kutoka kwa Data Wallet ilitaja kwamba Binance amepigwa marufuku nchini Uingereza na Mamlaka ya Maadili ya Kifedha kutokana na kufanya shughuli zozote zilizodhibitiwa.
Binance pia imepigwa marufuku nchini Japan, Canada, Malaysia, Bangladesh, Ufaransa, Thailand, Kazakhstan, Vietnam, Uholanzi, Ubelgiji, Italia, Ufilipino, Australia, Iran, India na Uchina.
Kwa kifupi, shughuli za Binance zimewekewa vikwazo katika zaidi ya nchi 19 duniani kote, jarida la Bankrate linabaini.
Bitcoin
Hii ni miongoni mwa kampuni za cryptocurrencies za awai kabisa kuingia katika masoko ya mataifa ya Afrika.
Hata hivyo, hio halikuwaweka katika nafasi salama ya kutojipata katika njia panda na kulazimishwa kuondoka katika baadhi ya mataifa kutokana na kutokidhi baadhi ya mahitaji muhimu.
Kwa sasa Algeria inakataza matumizi ya sarafu ya Bitcoin kufuatia kupitishwa kwa sheria ya fedha mwaka wa 2018 iliyofanya kuwa kinyume cha sheria kununua, kuuza, kutumia au kushikilia sarafu pepe, Euro News walisema.
Mataifa mengine yaliyokwamisha uhusiano wao na Bitcoin katika mataifa yao ni pamoja na Bolivia, Bangladesh, Misri, Uchina, Kolombia, Indonesia, Ghana, Iran, India miongoni mwa mengine.
Makedonia Kaskazini ndiyo nchi pekee ya Ulaya iliyopiga marufuku rasmi fedha za siri, kama vile Bitcoin, Ethereum na nyinginezo huku Nepal wakiharamisha biashara ya Bitcoin mapema 2017.
Dogecoin
Dogecoin iliundwa mwaka wa 2013 kama mbishi wa bitcoin, lakini cryptocurrency imekuwa uwekezaji halali kwa wafanyabiashara wengi wa crypto kwa sababu ya unyenyekevu wake, wafuasi wake wa hali ya juu akiwemo bilionea wa X na Tesla, Elon Musk.
Hata hivyo, Dogecoin imepigwa marufuku kaitka baadhi ya mataifa yakiwemo, China, Uturuki, Bangladesh, Urusi, India, na Indonesia.