Madereva walifanya majaribio ya magari siku ya Jumatano katika eneo la Loldia, Naivasha kabla ya mbio za magari za mwaka huu nchini Kenya kuanza.
Mashindano hayo ambayo yalizinduliwa na rais William Ruto katika KICC siku ya Alhamisi yatakamilika katika Hell’s Gate siku ya Jumapili.
Wakati wa majaribio, madereva hujaribu mipangilio mbalimbali kwenye magari yao kabla ya mbio.
Karan ndiye alikuwa Mkenya aliyeongoza kwa majaribio huku akichukua nafasi ya 14 kwa kasi huku Tundo na Samman wakiibuka wa 17 na 18 mtawalia.
Mashindano ya WRC-2 yamewavutia madereva mashuhuri barani Ulaya miongoni mwao Brit Gus Greensmith na Kajetan Kajetanowicz ambao wote wataanza raundi ya Kenya nyuma ya gurudumu la Skoda Fabia RS Rally2s.
Greensmith alimpita mshindani mwenzake wa Toksport Oliver Solberg kwa sekunde 1.2.
Bingwa wa Kenya Jasmeet Chana alijiondoa kwenye hafla hiyo kufuatia kuchelewa kwa gari lake la Ford Fiesta kutoka Ulaya.
Tazama picha za tukio hilo: