logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Idadi ya maafisa wa polisi wanaotakikana kwenda Haiti yaongezwa kutoka 1,000 hadi 5,000

Alhamisi, alisema hali ni mbaya zaidi kwamba idadi hiyo maradufu na zaidi inahitajika.

image
na Davis Ojiambo

Habari31 March 2024 - 12:04

Muhtasari


  • • Julai iliyopita, O’Neill alisema Haiti ilihitaji kati ya polisi 1,000 na 2,000 wa kimataifa waliofunzwa kukabiliana na magenge.
  • • Alhamisi, alisema hali ni mbaya zaidi kwamba idadi hiyo maradufu na zaidi inahitajika kusaidia Polisi wa Kitaifa wa Haiti kurejesha udhibiti wa usalama .
Makurutu wa polisi

Haiti sasa inahitaji kati ya polisi 4,000 na 5,000 wa kimataifa kusaidia kukabiliana na ghasia "mbaya" za magenge ambayo yanalenga watu muhimu na hospitali, shule, benki na taasisi nyingine muhimu, mtaalam wa haki za Umoja wa Mataifa wa taifa hilo lililokumbwa na migogoro la Caribbean, William O’Neill alisema Alhamisi kwa mujibu wa AP.

Julai iliyopita, O’Neill alisema Haiti ilihitaji kati ya polisi 1,000 na 2,000 wa kimataifa waliofunzwa kukabiliana na magenge.

Alhamisi, alisema hali ni mbaya zaidi kwamba idadi hiyo maradufu na zaidi inahitajika kusaidia Polisi wa Kitaifa wa Haiti kurejesha udhibiti wa usalama na kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, O'Neill alizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari akizindua ripoti ya Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa aliyosaidia kutoa ambayo ilitaka hatua za haraka zichukuliwe ili kukabiliana na hali ya "janga" nchini Haiti ambapo rushwa, kutokujali na utawala mbovu unaochangiwa na ongezeko la ghasia za magenge kumemomonyoa utawala wa sheria na kuleta taasisi za serikali "karibu na kuanguka."

Ripoti hiyo iliyoangazia kipindi cha miezi mitano kinachoishia Februari, ilisema magenge yanaendelea kuwasajili na kuwanyanyasa wavulana na wasichana, huku baadhi ya watoto wakiuawa kwa kujaribu kutoroka.

Haya yanajiri wakati ambapo taarifa mpya zinaarifu kwamba Jumakosi, wanaume wawili nchini Haiti waliuawa kwa kukatwakatwa na kundi la watu waliodhani walikuwa wakinunua risasi au bunduki kwa ajili ya magenge ambayo yameitikisa nchi hiyo, polisi walisema Jumamosi.

Kwa mujibu wa Washington Post, Polisi walithibitisha kuwa watu hao waliwanyakua watu hao kutoka mikononi mwa polisi baada ya kupatikana na takriban dola 20,000 na sawa na takriban dola 43,000 za pesa taslimu za Haiti kwenye gari lao, pamoja na bastola mbili na sanduku la risasi.

Kubeba kiasi hicho cha pesa kulichukuliwa kuwa jambo la kutiliwa shaka, na wakaaji walidhani ni ununuzi wa silaha kwa magenge hayo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved