logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DP Gachagua amtembelea hospitalini polisi aliyechomwa mshale na mgema pombe haramu

Afisa huyo na wenzake walikuwa katika msako dhidi ya pombe haramu mjini Thika.

image
na Davis Ojiambo

Habari03 April 2024 - 10:25

Muhtasari


  • • Aliandamana na Seneta wa Kiambu Karungo Thangwa na Mbunge wa Juja George Koimburi miongoni mwa viongozi wengine.
DP Gachagua akimtembelea polisi aliyeshambuliwa

Jumanne alasiri, naibu wa rais Rigathi Gachagua alimtembelea OCS wa polisi wa Juja aliyeripotiwa kushambuliwa kwa mshale na mgemaji wa pombe haramu huko Thika.

Gachagua alikuwa akizungumza baada ya kumtembelea OCS wa Kituo cha Polisi cha Juja, Inspekta Mkuu John Misoi, ambaye anapokea matibabu katika Hospitali ya Avenue mjini Thika kufuatia shambulio la watengenezaji pombe na wauzaji wa pombe haramu ya kuua watu huko Kiambu.

Aliandamana na Seneta wa Kiambu Karungo Thangwa na Mbunge wa Juja George Koimburi miongoni mwa viongozi wengine.

Naibu wa rais ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kupambana dhidi ya uuzaji wa pombe haramu katika eneo la Mlima Kenya alimwambia polisi huyo kwamba alimtembelea ili kumpa moyo.

“Tunakutakia mema, hii ni kadi kwako kuhisi nafuu, utakuwa sawa, ujue kwamba tunakuthamini, unajua mageuzi ambayo tunazidi kusukuma kuhusu bima ya afya kwa maafisa wa polisi ambao wanajeruhiwa wakiwa katika majukumu yao na mambo mengine yote tunayofanya kuhakikisha huduma ya polisi inakuwa afadhali,” Gachagua alisema.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved