Mahakama ya Katiba ya Uganda imeidhinisha sheria yenye utata dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, ambayo inatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela na adhabu ya kifo kwa wale wanaojihusisha na baadhi ya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.
Lakini mahakama ilidhoofisha sheria hiyo, ikisema kuwa baadhi ya sehemu zilikiuka haki za kikatiba.
Sehemu zinazoharamisha tabia kama vile kuruhusu ngono kwa wapenzi wa jinsia moja kutokea katika jengo la mtu, kushindwa kuripoti vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kumpa mtu ugonjwa usiotibika kupitia ngono ya mapenzi ya jinsia moja zitakabiliwa.
"Tunakataa kubatilisha Sheria ya Kupambana na Mapenzi ya jinsia moja 2023 kwa ujumla wake, wala hatutatoa amri ya kudumu dhidi ya utekelezaji wake," jaji mkuu Richard Buteera alisema wakati wa uamuzi huo Jumatano.
Wanaopinga wanasema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Ombi la kubatilisha sheria hiyo liliwasilishwa na wanataaluma wa Uganda, wanaharakati wa haki za binadamu, wanasheria, waandishi wa habari, wabunge na viongozi wa dini.
Walisema kuwa sheria hiyo inakiuka haki za kimsingi zinazotolewa na katiba, kama vile haki ya faragha na uhuru wa kutobaguliwa.
Waliongeza kuwa sheria hiyo ilikiuka ahadi za nchi chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.
Licha ya wasiwasi kama huo, sheria hiyo imeungwa mkono kwa kiasi kikubwa nchini humo. Wabunge wamewashutumu wapinzani katika nchi za Magharibi kwa kujaribu kuishinikiza Afrika kukubali mapenzi ya jinsi moja.