logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mgonjwa aliyepandikizwa figo ya nguruwe atoka hospitali

Katika taarifa, Bw Slayman amepokwa kwa furaha uamuzi wa madaktari kumruhusu kuondoka hospitalini.

image
na Samuel Maina

Habari04 April 2024 - 11:47

Muhtasari


  • •Mtu huyo mwenye umri wa miaka 62 aliruhusiwa kwenda nyumbani, wiki mbili baada ya upasuaji wa dharura katika Hospitali Kuu ya Massachusetts (MGH).
  • •Katika taarifa, Bw Slayman amepokwa kwa furaha uamuzi wa madaktari kumruhusu kuondoka hospitalini.

Mwanaume wa kwanza kupandikizwa figo iliyobadilishwa vinasaba kutoka kwa nguruwe ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 62 aliruhusiwa kwenda nyumbani, wiki mbili baada ya upasuaji wa dharura katika Hospitali Kuu ya Massachusetts (MGH).

Upandikizaji wa viungo kutoka kwa nguruwe waliobadilishwa vinasaba haukufanikiwa siku za nyuma.

Lakini mafanikio ya utaratibu huu hadi sasa yamesifiwa na wanasayansi kama hatua ya kihistoria katika uwanja wa upandikizaji.

Katika taarifa, hospitali ilisema mgonjwa, Richard "Rick" Slayman wa Weymouth, Massachusetts, alikuwa akipambana na ugonjwa wa figo na alihitaji kupandikizwa kiungo hicho ili kuokoa maisha yake.

Madaktari wake walifanikiwa kupandikiza figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba katika mwili wake katika upasuaji ulifanyika kwa saa nne tarehe 16 mwezi Machi.

Walisema figo ya Bw Slayman sasa inafanya kazi vizuri na kwamba hahitaji kufanyiwa tiba ya dialysis.

Katika taarifa, Bw Slayman amepokwa kwa furaha uamuzi wa madaktari kumruhusu kuondoka hospitalini.

Ni "mojawapo ya nyakati za furaha" maishani mwake, alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved