Rais William Ruto wikendi iliyopita aliwavunja mbavu waumini wa kanisa la ACK huko Nyeri baada ya kutaja zawadi ambayo atamnunulia askofu anayeenda kustaafu.
Ruto alikuwa miongoni mwa mamia ya waumini wa ACK ambao walimiminika kaitka kanisa la Kiangilikana la St Peter’s Cathedral huko Nyeri kwa hafla ya kumsherehekea askofu Joseph Kagunda ambaye anaenda kustaafu.
Kagunda amekuwa askofu wa ACK tawi la Magharibi mwa mlima Kenya kwa miaka 20 na alisherehekewa wakati anajiandaa kukabidhi majukumu ya kanisa kwa uongozi mpya ambao umetajwa kuzozaniwa na wengi.
Wakati wa hotuba yake, Rais Ruto alitania kwamba alikuwa analenga kumnunulia Kagunda gari kama zawadi ya kustaafu lakini baada ya kubaini kwamba waumini walishamtekelezea hilo, alisema alibadli wazo lake na kutaka kumnunulia toroli.
“Ahsanteni sana kwa huyu rafiki yangu askofu Kagunda, nilikuwa nafikiri nitamnunulia ari lakini nyinyi mmefanya kazi nzuri mmemnunulia gari. Sasa ile kazi imebaki, mimi nitamnunulia wheelbarrow,” Ruto alisema huku waumini wakicheka na kumlazimu kucheka pia.
Kiongozi wa taifa aliendelea kumwambia askofu huyo kwamba wiki ijayo anafaa kumtembelea kumuona akitania Zaidi kwamba pale atakuwa amejipanga vizuri na zawadi yake ya toroli.
Hii hapa video ya rais Ruto akitoa ahadi hiyo;