Mastaa wa media wazungumzia nyakati zao na marehemu Micheal Oyier

Aliyetajwa kuwa gwiji ambaye aliongoza na kuibua vipaji vya vijana kwenye vyombo vya habari wakati akiwa hai.

Muhtasari
  • Maneno mazuri ya kumuomboleza yalmiminika muda mfupi baada ya habari za kifo chake kugonga vichwa vya habari.
Marehemu Michael Oyier
Image: HISANI

Hadi kufikia kifo chake, Michael Oyier alikuwa gwijii wa utangazaji ambaye alipamba skrini kwa utulivu, maneno ya hadithi, ufasaha na neema huku akigusa maisha ya watu wengi  enzi za uhai wake. 

Haya yalijidhihirisha wazi katika maneno mazuri ya kumuomboleza yaliyomiminika muda mfupi baada ya habari za kifo chake kugonga vichwa vya habari huku wenzake wa zamani wakimpongeza kwa heshima kubwa.

Aliyetajwa kuwa gwiji ambaye aliongoza na kuibua vipaji vya vijana kwenye vyombo vya habari wakati wa enzi yake, mtangazaji huyo wa zamani wa KTN alisherehekewa kwa sifa kadhaa ambazo zilimfanya aonekane.

Mtangazaji wa redio Maina Kageni alimuomboleza, akimshukuru Oyier kwa pamoja na mambo mengine, yake;  kujitolea, nidhamu na uandishi wa kutia moyo;

"Tumepoteza legendari. Asante kwa kila kitu Michael Oyier...Mmoja wa watangazaji bora sana wa habari ambao nimewahi kuwafahamu..... Mfano wa kweli wa kujitolea, nidhamu na kutia moyo!!! Pole za dhati kwa wanahabari wote ndugu. na familia na marafiki Pumzika kwa Amani Michael Oyier."

Joy Doreen Biira ambaye alifanya kazi pamoja na Oyier katika KTN alimkumbuka kwa maadili bora ya kazi na wema wake, akibainisha kuwa habari za kifo chake ziligusa pakubwa.

"Mike alikuwa na maadili ya ajabu ya kazi. Alikuwa mkarimu, mwenye umakini, mwenye heshima, rafiki. Kila aliporipoti kazini, alikuwa akisalimia kila mfanyakazi mwenzake. Alikuwa akitoa vidokezo na ushauri wote. Ningeuliza vivyo hivyo na yeye pia alishiriki mengi yake, kisha tungepitia taarifa za habari pamoja. Alikuwa mwangalifu kwani alikuwa wa kimataifa kuhusu kile alichotaka kueleza. Nilipata kujifunza baadaye kuwa alikuwa mshauri halisi." Joy Doreen aliandika.

Mashirima Kapombe: Inasikitisha sana kwamba hatuwezi kupata mapumziko na kifo. Raha ya milele umpe Michael Oyier, Ee Bwana, na mwanga wa milele umuangazie. Naomba RIP. Amina!

Esther Muthoni Passaris: Michael Oyier alikuwa mwanahabari mwenye shauku na mtangazaji bora. Pole zangu za dhati kwa familia na marafiki zake

Ripoti zinaonyesha kuwa Oyier alianguka nyumbani kwake Lavington baada ya kulalamikia maumivu makali ya kichwa siku ya Jumatano na kukimbizwa hospitalini.

Kulingana na familia yake, mwanahabari huyo aliaga dunia saa 2:30 usiku alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi na mwili huo kuhamishwa katika Makao ya Mazishi ya Lee ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa maiti.