logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Video ya muuguzi akichukua selfie na mjamzito katika maumivu ya leba yavutia hisia mseto

Licha ya masikini huyo kulia kwa uchungu, muuguzi huyo hata hivyo aliendelea kufanya video.

image
na Radio Jambo

Habari02 May 2024 - 10:40

Muhtasari


β€’ Licha ya masikini huyo kulia kwa uchungu, muuguzi huyo hata hivyo aliendelea kufanya video ya mwanamke huyo mjamzito na kutabasamu.

Nesi akijirekodi kwenye wadi ya leba

Video ya kutatanisha ya muuguzi wa kike akipuuza majukumu yake kwa mtindo wa maisha ya mitandao ya kijamii imekuwa ikienea mtandaoni na kwa kuongeza, ilizua gumzo pevu.

Mama mjamzito, anayeonekana kukaribia kujifungua, alionekana akiwa hana raha kwenye kitanda cha hospitali, lakini nesi, aliyeketi kando yake, aliamua kutumia tukio hilo la kusikitisha kuunda maudhui ya kujifaidi mitandaoni badala ya kumsaidia.

Katika klipu hiyo iliyosambazwa mtandaoni, muuguzi huyo, akiwa amevalia sare ya majukumu yake ya kijani kibichi, alionekana akipiga video ya selfie na mwanamke mjamzito katika leba.

Licha ya masikini huyo kulia kwa uchungu, muuguzi huyo hata hivyo aliendelea kufanya video ya mwanamke huyo mjamzito na kutabasamu.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii, waliotazama video hiyo, walionyesha hasira zao kwa muuguzi huyo, ambaye alichagua kuacha majukumu yake ili kuunda maudhui.

Wengine walimtetea nesi huyo wakidai huenda ni familia ya mwanamke huyo au hata yeye mwenyewe alimtaka kurekodi matukio ya kabla ya kujifungua kwa faida yake baada ya kuenda nyumbani.

Tazama video hiyo hapa chini kisha utoe maoni yako;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved