Msemaji wa serikali Isaac Mwaura amewahakikishia Wakenya kuwa yuko salama baada ya chopa aliyokuwa akisafiria kutua kwa dharura huko Gishungo, eneo bunge la Kikuyu.
Kulingana na Mwaura, kutua huko kulitokana na hali mbaya ya anga.
Alikuwa na katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya Idriss Ahmed.
Wawili hao, miongoni mwa viongozi wengine, waliyokuwa wakirejea kutoka Nyando, kaunti ya Kisumu, ambako walikuwa wameenda kupeleka bidhaa zisizo za chakula kwa wakazi ambao walikuwa wamehamishwa na mafuriko.
"Mimi niko salama Wakenya wenzangu. Ndege yetu ililazimika kutua kwa dharura huko Gishungo, Jimbo la Kikuyu kutokana na hali mbaya ya hewa. Idriss Ahmed Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na mimi tulikuwa tumeenda Nyando huko Kisumu kutoa msaada kwa wasio-- Bidhaa za Chakula (NFIs) kwa Watu Walioathiriwa na Mafuriko (FAPs).
"Tulifika nyumbani salama na tunamshukuru Mungu kwa hili. Heri ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani," alisema.
Katika video iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii, Mwaura anasikika akiwaeleza wakazi kilichojiri na kuendelea kuwataka waitunze chopa hiyo hadi itakapokuwa salama kuondoka.
Mwaura na Idriss walitoa afueni kwa watu 441 walioathiriwa na mafuriko katika Shule ya Sekondari ya Nduru mnamo Jumanne.
Mwaura amekuwa akizunguka nchi nzima kutathmini hali ya mafuriko na kusambaza misaada kwa wakaazi walioathirika zaidi.
Katika baadhi ya matukio, wamekuwa wakisambaza vitu muhimu vya chakula na visivyo vya chakula kwa walioathirika.