Wizara ya Afya (MOH) imetoa vidokezo vya usalama kusaidia wananchi huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha maeneo mengi ya nchi na kusababisha mafuriko makubwa.
Katika ushauri uliotolewa Jumatano, Mei 8, MOH ilisisitiza umuhimu wa kukaa salama wakati wa mvua inayoendelea na uwezekano wa mafuriko.
Moja ya ushauri kutoka kwa wizara ni kwa watu binafsi kuchukua tahadhari wanapokutana na barabara zilizojaa maji.
"Ukikutana na barabara hiliyo na maji mengi geuka," sehemu ya ushauri inasema
Zaidi ya hayo, Wizara ya Afya iliwataka wananchi kubaki ndani na mbali na madirisha wakati wa mvua kubwa ili kupunguza uwezekano wa hatari.
Kutembea au kuendesha gari kwenye maji ya mafuriko hakukubaliwi sana kwani kunaweza kusababisha hatari kubwa kwa usalama wa kibinafsi.
Wizara imependekeza watu katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko kuhama katika maeneo salama.
Wananchi walishauriwa kuwaangalia majirani zao, hasa wazee au wale wenye mahitaji maalum.
Zaidi ya hayo, watu binafsi walishauriwa kujiepusha na kutafuta makazi chini ya miti wakati wa mvua, kwani inaweza kuongeza hatari ya kupigwa na radi au matawi kuanguka.