logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume akiri kuwaua watalii watatu waliotoweka Mexico

Mpenzi wake Ari Gisel na mwanamume mwingine wamezuiliwa kwa kushukiwa kuhusika.

image
na Samuel Maina

Habari09 May 2024 - 04:13

Muhtasari


  • •Ndugu wa Australia Jake na Callum Robinson na rafiki yao Mmarekani Jack Carter Rhoad walitoweka tarehe 27 Aprili karibu na Ensenada.
  • • Mpenzi wake Ari Gisel na mwanamume mwingine wamezuiliwa kwa kushukiwa kuhusika.

Mwanamume aliyeshtakiwa kwa kutoweka kwa watalii watatu katika safari ya kuteleza kwenye mawimbi nchini Mexico alikiri kuwaua, mahakama imesikiliza ushahidi huo.

Ndugu wa Australia Jake na Callum Robinson na rafiki yao Mmarekani Jack Carter Rhoad walitoweka tarehe 27 Aprili karibu na Ensenada.

Jesús Gerardo Jumatano alikabiliwa na mahakama kwa makosa ya utekaji nyara, lakini maafisa wanasema mashtaka ya mauaji yatafunguliwa hivi karibuni.

Pia anajulikana kama "El Kekas", bado hajawasilisha ombi.

Maafisa wa jimbo la Baja California wamesema watalii hao watatu - wote wakiwa na umri wa miaka ya 30 - huenda waliuawa walipokuwa wakijaribu kuzuia wizi wa matairi ya lori lao la kubebea mizigo.

Miili yao ilipatikana ikiwa imetupwa kwenye kisima cha miamba siku sita baada ya kutoweka, kila mmoja akiwa na risasi kichwani, kulingana na mamlaka za eneo hilo. Mwili wa nne pia ulipatikana kwenye kisima hicho lakini ulikuwa hapo kwa muda mrefu na haukujumuishwa kwenye kesi hiyo, waliongeza.

Jesús ameshtakiwa kwa "kutoweka kwa lazima" na mpenzi wake Ari Gisel na mwanamume mwingine wamezuiliwa kwa kushukiwa kuhusika. Majina yao ya ukoo yamefichwa na mahakama.

Wakati wa kufikishwa mahakamani Jumatano, waendesha mashtaka walimtaja Ari - ambaye hajafunguliwa mashtaka kuhusu kutoweka kwao - kama mmoja wa mashahidi wao.

Mahakama iliambiwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 aliwaambia wachunguzi kwamba Jesús alifika nyumbani kwake tarehe 28 Aprili, na kumwambia kuwa alikuwa amefanya kitu kwa watu watatu.

Alimuuliza anamaanisha nini, naye akajibu "nimewaua", kikao kiliambiwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved