logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Goodluck Jonathan ana wasiwasi kuhusu utaratibu wa upigaji kura Afrika Kusini

"Elimu ya wapiga kura itahitaji kufanyika hata katika vituo vya kupigia kura, jambo ambalo litapunguza kasi ya mchakato huo," anasema.

image
na Samuel Maina

Habari29 May 2024 - 12:54

Muhtasari


  • •Jonathan ambaye anaongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi nchini Afrika Kusini, anasema ana wasiwasi kuhusu taratibu mpya za usajili nchini humo.
  • •"Elimu ya wapiga kura itahitaji kufanyika hata katika vituo vya kupigia kura, jambo ambalo litapunguza kasi ya mchakato huo," anasema.

Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, ambaye anaongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi nchini Afrika Kusini, anasema ana wasiwasi kuhusu taratibu mpya za usajili nchini humo.

"Tulichokuwa na wasiwasi nacho ni watu ambao hawajaenda katika majimbo yao kupiga kura," anaiambia BBC.

"Siku za nyuma, wapiga kura wangeweza kupiga kura zao katika miji mikubwa kama Pretoria, Johannesburg au Cape Town bila usumbufu mwingi.

"Hata hivyo, wakati huu, wapiga kura walihitaji kutuma maombi kwa tume ya uchaguzi kwa ajili ya kupangiwa kama walitaka kupiga kura nje ya jimbo lao lililosajiliwa."

Jonathan, ambaye aliongoza Nigeria kutoka 2010 hadi 2015, anasema wapiga kura wengi hawakuwa wamekamilisha mchakato huu, wakiamini wanaweza kupiga kura kama hapo awali.

Jonathan, mwenye umri wa miaka 66 pia anasema "mkanganyiko juu ya kuanzishwa kwa kura hiyo, hatua inayolenga kutoa fursa hata kwa wagombea binafsi kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, inaweza pia kuwa na athari.

"Elimu ya wapiga kura itahitaji kufanyika hata katika vituo vya kupigia kura, jambo ambalo litapunguza kasi ya mchakato huo," anasema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved