Chama cha aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kinajaribu kuzuia shughuli ya kutangaza matokeo zisifanyike kama ilivyopangwa kikitaka marudio ya uchaguzi wa juma lililopita.
Tume ya uchaguzi haitaweza kukubaliana na hili, na inasonga mbele kutangaza matokeo ya mwisho baadaye leo.
Matakwa ya chama cha MK cha Bw Zuma yanakuja ghafla.
Alikuwa mshindi mkubwa zaidi wa uchaguzi huo, akishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa kitaifa. Lakini ilishindwa kupata wingi wa kura katika jimbo analotoka Bw Zuma la KwaZulu-Natal.
Hili ni pigo kubwa kwa chama, kwani kitalazimika kutafuta mshirika wa muungano iwapo kitataka kuliongoza jimbo hilo.
Hii inaweka kikomo chaguo la Bw Zuma la kutumia KwaZulu-Natal kama ngome ya kupigana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, na kulazimisha kujiuzulu.
Hilo ndilo lengo kuu la Bw Zuma. Bw Ramaphosa alimtimua kama rais mwaka wa 2019, na sasa anataka kulipiza kisasi.