Chuo Kikuu cha Palermo nchini Italia kilitangaza siku ya Jumanne, kususia uhusiano wowote wa kitaaluma na vyuo vikuu vya Israeli hadi mwisho wa vita vya Israeli dhidi ya Gaza.
Uamuzi wa Baraza la Kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Palermo (kilichoanzishwa mnamo 1806) kusitisha makubaliano yake na vyuo vikuu vya Israeli unafuatia kile walichoelezea kama "ukosefu wa dhamana muhimu za usalama ambazo washiriki waliotumwa watakabiliwa nazo katika wakati huu nyeti wa mzozo wa kimataifa."
Baraza pia lilitangaza azma yake ya kuchukua hatua zinazolenga kusaidia mfumo wa elimu wa Palestina.
Kwa upande wao, waandamanaji wanaotaka kukatishwa kwa uhusiano na vyuo vikuu vya Israeli waliona kuwa uamuzi wa chuo hicho unatimiza matakwa ambayo ndiyo chanzo cha kuandaa maandamano hayo.
Ni jambo la kustaajabisha kuwa Ulaya, Marekani na nchi nyinginezo zinashuhudia ongezeko la maandamano ya wanafunzi kuunga mkono Palestina.
Maandamano haya yanatoa wito wa kukomeshwa kwa vita vya Israel dhidi ya Gaza, na pia kutaka kuondolewa kwa uwekezaji au mahusiano yoyote ambayo vyuo hivi vikuu vinavyo na makampuni ya Israel.
Vilevile wanayaona makampuni haya kuwa yamehusika kwenye vita vya maangamizi vilivyoanzishwa na wanajeshi wa Israeli kwenye ukanda wa Gaza kwa zaidi ya takriban miezi minane sasa.
Vita vya Israeli dhidi ya Gaza viliacha zaidi ya mashahidi 119,000 wa Kipalestina na majeruhi kadhaa ambao wengi wao ni watoto na wanawake wajawazito. Takriban watu 10,000 walipotea, huku kukishuhudiwa na uharibifu mkubwa wa mali.
Uharibifu huu umesababisha njaa iliyogharimu maisha ya watoto na wazee. Israel inaendeleza vita hivi, ikipuuza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloitaka kusitisha mapigano mara moja.
Vyuo hivi vimeagiza kutolewa kwa amri kutoka kwa Mahakama ya Haki vikitaka Israeli ikomeshe mashambulizi yake dhidi ya Rafah
Pia, wamedai kuchukuliwa kwa hatua za haraka upesi ili kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki na kuboresha hali ya kibinadamu huko Gaza.