logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Seneta Omtatah amuonya rais kuwa makini asijipate mashakani

Wakenya waelekeze mawazo kwa kile alichotaja kama "ufisadi wa bajeti" utakaogharimu nchi takriban shilingi bilioni mia moja

image
na Davis Ojiambo

Habari06 June 2024 - 07:07

Muhtasari


  • •Rais asipofuata hati ya kisheria ya nchi katika utekelezaji wa mambo ya serikali anaweza jipata mbaroni baada ya muhula wake
  • •"ndani ya katiba hii zipo hatua za kuwaadhibu watu hawa (serikali)," seneta Omtatah
  • •"Lazima atii Katiba, hakuna namna nyingine,"aliendela Omtatah

Seneta wa Busia Okiya Omtatah amemuonya rais William Ruto vikali kufuatia namna anavyoendesha nchi na na kutekeleza sera zake.

Akizungumza na Citizen Tv mnamo Jumatano jioni, Omtatah alimkanya rais dhidi ya kutumia mamlaka yake vibaya kwani anaweza kipata chuma chake ki motoni na sheria za katiba ya nchi baada ya kukamilisha muhula wake kama rais.

Kulingana na seneta Okiya Omtata, rais akizidi kutia komango kwa kutojua mara kwa mara hati ya kisheria ya nchi katika ukamilishaji na utekelezaji wa mambo ya serikali kunaweza mtia mbaroni baada ya kukamilisha muhula wake.

Fauka ya hayo, alimshauri rais Ruto atilie maanani kwa kuzingatia idadi ya marais waliostaafu na baadaye kufungwa nchini Korea Kusini, ambako yuko kwa sasa katika ziara rasmi.

Vile vile, Omtatah alitaja hali kuwa "mbaya" kwa rais na hivyo basi kumrai awe makini wakati yupo madarakani.

“Tuna katiba rasmi katika taifa letu, na ndani ya katiba hii zipo hatua za kuwaadhibu watu hawa (serikali). Utawadia wakati ambapo tutawatia gerezani kwa dhuluma wanazofanya leo," Omtatah alisema.

“Rais Ruto yumo Korea Kusini, ajiulize mwenyewe, ni marais wangapi wa zamani wa Korea Kusini wameenda jela? Anapofurahia mandhari Korea Kusini, lazima ang'amue kuwa upo upande ambapo marais wakorofi wanafungwa jela na kuadhibiwa vilivyo."

"Je, rais Ruto anataka kufungwa jela akiondoka madarakani? Hilo ndilo swali analopaswa kujiuliza. Lazima atii Katiba, hakuna namna nyingine."

Seneta huyo aliendelea kutaja Mswada wa Fedha wa mwaka 2024 unaoendelea kuibua mdahalo mkali kama mbinu kigeugeu ya serikali kuzuia wakenya kuzingatia madai ya uporaji unaoendelea kufichwa kwenye bajeti.

Kulingana na Omtatah, wakenya wanapaswa kwa wakati huu kuuchukulia Mswada wa Fedha kama sio suala kuu, na badala yake waelekeze mawazo yao kwa kile alichotaja kama "ufisadi wa bajeti" ambao utagharimu nchi takriban shilingi bilioni mia moja.

Aliongezea kuwa ufisadi huu umekithiri mno kwani, mswada huu umetenga bilioni mia moja katika ulipaj wa deni ilhali ni shilingi bilioni sitini inayohitajika. Pia, serikali imetenga bilioni hamsini na mbili katika gharama nyingine ambazo zinaleta mushkili na tashwishi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved