KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Juni 7.
Katika taarifa ya siku ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa maeneo kadhaa ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme Ijumaa ni pamoja na Uasin Gishu, Kisii, na Kiambu.
Katika kaunti ya Uasin Gishu, baadhi ya sehemu za eneo la Kapseret Lemook zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Nyamataro, Nyakoe, na Mosocho katika kaunti ya Kisii zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa tisa alasiri.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kiambaa na Waguthu katika kaunti ya Kiambu pia zitathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.