KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Juni 11.
Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Kiambu, Nyeri, Murang'a, Uasin Gishu, Busia, Kisii, Homa Bay, na Kitui.
Katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kenyatta Road, Murrum, Slopes Villa, na Izaak Walton zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Tetu, Gitero, na Muthuaini katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Gatitu, na Gaichanjiru katika kaunti ya Murang'a zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Uasin Gishu, eneo la Moi University Main Campus litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Busia, sehemu kadhaa za mji wa Malaba na Amagoro zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Embonga na Lepremier katika kaunti ya Kisii zitakosa umeme kati ya saa moja na dakika ishirini asubuhi na saa saba na dakika ishirini mchana.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Ndisi na Kodumbe katika kaunti ya Homa Bay zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Kwa Vonza, Kyusiani, na Kauwongo katika kaunti ya Kitui pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.