Kampuni ya kusambaza umeme nchini Kenya,Kenya Power imewaagiza wateja wake wa malipo ya umeme kusasisha mita zao, zinazojulikana kama tokeni mita, kufikia Agosti ili kuendelea kupata umeme.
Kampuni hio ya kusambaza umeme imesema kuwa sasisho la kimataifa linaloendelea la mita zote za kulipia ambazo hutumia vigezo vya kawaida vya uhamisho itahakikisha usalama wa tokeni zinazozalishwa. Jumla ya mita za malipo takriban milioni 7.4 zimelengwa kwa zoezi hili.
Mita zote za kulipia ambazo hazitakuwa zimesasishwa kufikia tarehe ya mwisho zitaacha kupokea tokeni baada ya tarehe ya makataa..Mkurugenzi mkuu wa Kenya Power Joseph Siror alisema.
Vile vile, wateja watapokea misimbo miwili [two codes] kupitia SMS kutoka kwa kampuni hio watakaponunua tokeni za umeme.
"Watahitajika kuweka misimbo kwenye mita zao kwa kufuata hatua zilizoonyeshwa kwenye SMS kabla ya kupakia tokeni mpya," Siror aliongoza.
"Katika hali zingine, kampuni itatuma misimbo moja kwa moja kwa wateja ambao hawajanunua tokeni ili kuwaarifu kusasisha mita zao. Mchakato ni rahisi na huru." Chapisho la taarifa lilidokeza.
Aidha kampuni hio ya kusambaza umeme ilisema kuwa sasisho hilo halitaathiri tokeni zilizopo za umeme ambazo tayari zimepakiwa kwenye mita za umeme. Wateja hata hivyo wameshauriwa kupakia tokeni zozote zilizonunuliwa hapo awali kabla ya kusasisha mita zao. Kenya Power ilisisitiza kuwa kukosa kufanya hivyo kutafanya vitengo vya umeme kuwa batili.