logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Marufuku ya ngono ya jinsi moja nchini Namibia ni kinyume cha katiba- Mahakama

Hakuna sheria zilizopo zinazokataza ngono kati ya wanawake nchini Namibia.

image

Habari22 June 2024 - 05:30

Muhtasari


  • Hukumu kwa makosa ya enzi ya ukoloni ya "ulawiti" na "makosa yasiyo ya asili ya ngono" zilikuwa nadra lakini zilichochea ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja ambao waliishi kwa hofu ya kukamatwa.
Mwanaharakati akipeperusha bendera ya kujivunia mashoga wakati wa maandamano huko Nairobi. Picha: MAKTABA

Katika uamuzi wa kihistoria kwa wanaharakati wa haki za watu wa mapenzi ya jinsi moja, sheria zinazopiga marufuku mapenzi ya jinsia moja kati ya wanaume zimeelezwa kuwa ni kinyume cha katiba nchini Namibia.

Hukumu kwa makosa ya enzi ya ukoloni ya "ulawiti" na "makosa yasiyo ya asili ya ngono" zilikuwa nadra lakini zilichochea ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja ambao waliishi kwa hofu ya kukamatwa.

Hakuna sheria zilizopo zinazokataza ngono kati ya wanawake nchini Namibia.

Ndoa za watu wa jinsia moja bado ni haramu katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Baada ya hukumu ya Ijumaa kusomwa katika mahakama kuu katika mji mkuu, Windhoek, wanaharakati wa kundi la LGBTQ la Equal Namibia walichapisha picha za watu wakiwa wamekumbatiana mahakamani.

Kesi hiyo mahakamani ililetwa na mwanaharakati wa Namibia anayeitwa Friedel Dausab, kwa kuungwa mkono na shirika la misaada la Uingereza la Human Dignity Trust.

"Haitakuwa kosa tena kupenda," Bw Dausab alisema akitoa maoni kuhusu hukumu hiyo, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa "alikuwa na furaha tu".

Umoja wa Mataifa pia umepongeza uamuzi huo, na kuuita "hatua yenye nguvu" kuelekea taifa shirikishi zaidi ambalo pia litaboresha upatikanaji wa huduma za afya na matibabu ya VVU.

Kwa kuhofia kurudishwa nyuma kwa uamuzi huo, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linaitaka serikali ya Namibia kuhakikisha usalama na utu wa watu wa LGBTQ.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved