logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi waanzisha uchunguzi kufuatia kifo tata cha mwanaume Siaya

Mwili wa marehemu ulikuwa na michubuko kwenye magoti yote mawili ambapo goti la kulia lilikuwa limefungwa na bandeji

image
na Davis Ojiambo

Habari24 June 2024 - 06:33

Muhtasari


  • •George Nyaginde Amenya mwenye umri wa miaka 25 alipatikana akiwa amepiga dunia teke ndani ya jikoni ya nina wake
  • •Mwili wa marehemu ulikuwa na michubuko kwenye magoti yote

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Siaya wamezindua uchunguzi kufuatia mauaji tata ya mkazi mmoja katika eneo la Ugenya.

George Nyaginde Amenya mwenye umri wa miaka 25 alipatikana akiwa amepiga dunia teke ndani ya jikoni ya nina wake.

Inaripotiwa kuwa, marehemu alishambuliwa Nyalenya kwenye gatuzi ndogo inayopatikana Uyunya.

Kulingana na kamishna wa polisi wa Siaya, Cleti Kimaiyo, kisa hiki kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha Aboke Patrol Base.

“Mkasa huu uliripotiwa na chifu wa gatuzi la Uyunya, Joachim Odhiambo Oyilo,” Kimaiyo alisema.

Maafisa wa polisi walizuru eneo la mkasa huo kwenye gatuzi ndogo la Nyalenya ambapo walipata mwili wa marehemu umeshapelekwa kwenye sebule ya mama yake.

Kimaiyo, vilevile, aliongeza kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na michubuko kwenye magoti yote mawili ambapo goti la kulia lilikuwa limefungwa na bandeji.

“Marehemu alikuwa chini ya matibabu baada ya kudaiwa kushambuliwa na watu ambao hawafahamiki vyema,” kamishna Kimaiyo aliongezea.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha kibinafsi kwenye mji wa Siaya ambapo uchunguzi wa maiti unatarajiwa kufanyika.    


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved