City Hall yawaka moto huku maandamano ya kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha yakizidi
Waandamanaji jijini Nairobi wamechoma Ikulu ya Jiji.
Video zilizoonekana na Radiojambo zilionyesha moshi mkubwa ukitoka kwenye jengo hilo.
Maafisa wa polisi walionekana wakizunguka jengo hilo.
Haya yanajiri saa chache baada ya waandamanji kuingia bunge na kuharibu baadi ya bidhaa katika jengo hilo.
Picha za Televisheni za moja kwa moja zinaonesha sehemu ya bunge ikiwa imeharibiwa vibaya.
Madirisha na viti vinaweza kuonekana vimevunjwa huku polisi wakiendelea kuwasukuma nje waandamanaji waliolifikia jengo hilo.