Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya amedai kwamba amepata mshahara wa mwezi Juni ukiwa chini ya shilingi za Kenya 2,400.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Salasya alichapisha picha ya payslip yake akionyesha jinsi mshahara wake ulipungua hadi kiasi hicho licha ya kuwa na jumla ya mshahara wa Zaidi ya shilingi milioni moja.
Katika payslip hiyo, Salasya, mwenye mshahara wa shilingi milioni 1.16 alionyesha jinsi makato kulipia mikopo ya vitu anavyomiliki na tozo mbalimbali zilivyouvamia mshahara wake na kuukata hadi chini ya 2,400.
Mbunge huyo mwenye vitimbi alisema kwamba yeye inambidi kuvumilia na mshahara huo mdogo, jambo ambalo alidai liliwashinda wabunge wenzake ambao walipiga kura ya kuupitisha mswada wa fedha 2024, akiashiria kwamba huenda walihongwa kutokana na jinsi mishahara yao inakuwa midogo kisa makato mengi ya mikopo na tozo.
Aidha, Salasya aliwasikitia baadhi ya wafanyikazi wa serikali kama walimu na polisi ambao mara nyingi hufanya kazi katka mazingira magumu na misharaha duni, akisema kama yake ikikatwa inashuka kutoka milioni hadi 2k, je ya wafanyikazi kama hao itakuwa inashuka hadi ngapi.
“Hii ndio salary yangu, hii ndio ilifanya wabunge wa kenya kwanza wakapiga yes kwa maneno kama hii sisi tulivumilia kama yangu inakaa hivi ya askari mwalimu na daktari zinakaa aje but nilivumilia haka ka payslip kangu,” Salasya alisema.
Wakati uo huo, tume ya kuratibu mishahara na marupurupu ya wafanyikazi wa serikali, SRC imetangaza kusitisha mpango wa kuwapa nyongeza wafanyikazi hao.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mwenyekiti wa tume hiyo Lyne Mengich alisema Jumatano kwamba tume ililazimika kubatilisha notisi ya nyongeza ya mishahara iliyochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali mwezi Agosti mwaka jana baada ya mashauriano ya kina na umma.
Wakati uo huo, tume ya kuratibu mishahara na marupurupu ya wafanyikazi wa serikali, SRC imetangaza kusitisha mpango wa kuwapa nyongeza wafanyikazi hao