KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Julai 6.
Katika taarifa ya Ijumaa jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Narok, Uasin Gishu, na Siaya.
Katika kaunti ya Narok, sehemu kadhaa za maeneo ya Sogoo, na Tendwet zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Sinendet Centre na Sakam Quarry katika kaunti ya Uasin Gishu zitakosa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Siaya, baadhi ya sehemu za maeneo ya Sagam na Lihanda pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.