Rais William Ruto amelivunja Baraza lake la Mawaziri na kuwarudisha nyumbani mawaziri wote na mwanasheria mkuu.
Uamuzi huo hauathiri Waziri Mkuu Musalia Mudavadi na naibu rais Rigathi Gachagua.
Hii hapa ni orodha ya waliotimuliwa;
Waziri Wizara
1.Kithure Kindiki Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa
2.Njuguna Ndung'u Wizara ya Hazina ya Kitaifa na Mipango
3.Aisha Jumwa Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi
4.Aden Duale Wizara ya Ulinzi
5.Alice Wahome Wizara ya Ardhi, Ujenzi wa Umma, Nyumba na Maendeleo ya Miji
6.Alfred Mutua, Wizara ya Utalii na Wanyamapori
7.Moses K. Kuria Wizara ya Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Utoaji
8.Rebecca Miano Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda
9.Kipchumba Murkomen Wizara ya Barabara na Uchukuzi
10.Zacharia Mwangi Njeru Wizara ya Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji
11.Peninah Malonza, Jumuiya ya Afrika Mashariki, 'The ASALs & Regional Development'
12.Mithika Linturi Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo
13. Ezekiel Machogu Wizara ya Elimu
14..Davis Chirchir Wizara ya Nishati na Petroli
15.Ababu Namwamba Wizara ya Masuala ya Vijana na Michezo
16.Simon Chelugui Wizara ya Ushirika na Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo na za Kati
17.Salim Mvurya Wizara ya Madini, Uchumi wa 'Bluu' na Masuala ya Bahari
18.Florence Bore Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii
19.Susan Nakhumicha Wafula Wizara ya Afya
20.Eliud Owalo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali
21.Roselinda Soipan Tuya Wizara ya mazingira na Misitu
22.Mercy Kiiru katibu wa baraza la mwaziri
23.Justin Muturi Mwanasheria mkuu wa serikali