logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Ruto kuondoka ofisini labda uchaguzi mwingine-Moses Kuria

Kuria alidokeza kuwa njia rahisi kwa vijana wa Kenya 'Gen Z ' ni kushiriki kwa kura ili kuondoa rais Ruto mwaka 2027.

image
na Davis Ojiambo

Habari11 July 2024 - 08:45

Muhtasari


  • •Moses Kuria alidai kuwa maandamano na usemi kuwa 'Rust must go' haitamwondoa rais Ruto ofisini ila ni kusubiri hadi uchaguzi mwingine ufanyike.
  • •Uchaguzi ujayo utafanyika mwaka 2027

Waziri wa utumishi wa umma Moses Kuria amesema kuwa Rais William Ruto anaweza tu kuondoka afisini kupitia uchaguzi mwingine.

Akiongea wakati wa mahojiano  kwenye  runinga ya Citizen TV  Jumatano, Kuria alisema kuwa rais hawezi kuondolewa kitini ikiwa hakuna uchaguzi.

Alithibitisha kuwa njia pekee ni njia ya kidemokrasia,hasa kwa vijana wa Gen Zs  kutumia nambari na sauti zao katika kupiga kura.

"Watu wanasema Ruto lazima aende lakini Ruto hakuja, alichaguliwa na uchaguzi mwingine unakuja. Njia pekee ya Ruto ni kupitia kura," alisema. Uchaguzi ujao nchini Kenya utafanyika mwaka wa 2027.

Kuria alisema hakuna haja ya nchi kutumbukia katika mapinduzi na ghasia, kama nchi nyingine za Afrika, akisema si mzaha bali ni usemi wa kichaa. Kuria aliendelea kusema njia pekee ya kumrudisha nyumbani ni kwa kutekeleza matakwa ya kidemokrasia ya wananchi.

“Jamani, angalieni upande wa pili, inaweza kuonekana kimahaba na maudhui mazuri lakini si mzaha,” alisema.

Waandamanaji wa Gen Z wamekuwa wakiimba kauli mbiu ya 'Ruto lazima aende' mitaani na mitandao ya kijamii. Miongoni mwa matakwa yao  ni kwamba Ruto ajiuzulu.

Kwa upande wake, Julai 3, Kuria alisema yuko tayari kukabiliana na matokeo ikiwa baraza la mawaziri la sasa litavunjwa. Kauli yake ilifuatia wito wa maseneta kumtaka Rais Ruto kuvunja baraza la mawaziri ili kukabiliana na changamoto za nchi.

"Iwapo mahakama itasema kwamba Moses Kuria lazima aende nyumbani, nitakuwa wa kwanza kusema ndio turudi nyumbani, lakini pia ni wakati mwafaka wa sisi pia kujifungua," Kuria alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved