Seneta wa Marsabit Mohammed Chute amekamatwa na maafisa kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC).
Msemaji wa EACC Eric Ngumbi amethibitisha kuwa Chute anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Integrity Center.
Seneta huyo anatuhumiwa kwa mgongano wa kimaslahi na anahusishwa na ufisadi wa mamilioni katika serikali ya kaunti ya Marsabit.
Kufuatia kukamatwa kwake, tume ya kukabiliana na ufisadi iliapa kuchunguza madai yaliyotolewa dhidi ya seneta huyo na kwamba maelezo zaidi yatatolewa kwa wakati ufaao.
Kukamatwa kwa Chute kunajiri siku moja tu baada ya kuandamana na Rais William Ruto wakati wa uzinduzi wa Kituo Kidogo cha Kimuka, Kajiado.
Wakati wa mkutano wake na Mkuu wa Nchi, Chute alimpongeza Rais kwa kutenga Ksh1 bilioni kwa ajili ya ufugaji wa mifugo kwa wafugaji katika kaunti ya Marsabit.