logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Orodha ya vitu vilivyopatikana kutoka kwa mshukiwa mkuu wa mauaji ya Kware

Alikamatwa Jumatatu asubuhi kutoka kwa maficho huko Kayole, mita 100 kutoka mahali ambapo miili ilipatikana.

image
na Davis Ojiambo

Habari15 July 2024 - 09:53

Muhtasari


  • •Kulingana na polisi, mshukiwa alikiri mauaji hayo ya mfululizo.
  • •Alikamatwa Jumatatu asubuhi kutoka kwa maficho huko Kayole, mita 100 kutoka mahali ambapo miili ilipatikana.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai Mohamed Amin amefichua orodha ya vitu vilivyopatikana na mshukiwa wa mauaji ya Kware.

Alipokamatwa, anaripotiwa kuwaongoza maafisa hadi katika chumba chake alichokodisha katika eneo la Kware, ambacho kiko takriban mita 100 kutoka eneo ambalo miili na sehemu za mwili zilipatikana.

"Msako wake na kukamatwa kwake kulifuatia uchunguzi wa kina wa simu ya rununu iliyokuwa ya mmoja wa waathiriwa Josephine Owino ambapo shughuli za pesa za rununu zilifanyika siku ambayo Josephine alitoweka," mkuu wa DCI alisema.

Kulingana na Amin, vitu kadhaa vimepatikana katika kwake ikiwa ni pamoja na sim card 24, simu 8 za kisasa, na simu mbili za sifa, laptop moja na hard drive moja.

Flash drives mbili na memory card, panga moja, ambalo maafisa wa upelelezi wanaamini lilikuwa likitumika kuwakata wahasiriwa, na magunia 12 ya nailoni sawa na yale yaliyotumika kujaza miili.

Glavu za mpira za viwandani, vitambulisho sita vya wanaume na vitambulisho viwili vya wanawake, mkoba mmoja wa kike , suruali mbili za kike , misokoto tano ya bangi, na sellotapes nne.

"Baadhi zilipatikana kwenye eneo la tukio."

Pia tulipata koti moja , hati miliki mbili, madaftari mawili .

"Wakati wa kuhojiwa, washukiwa walikiri  kuwaua na kutupa miili ya wanawake 42. Wote waliuawa kati ya 2022 na hivi majuzi Julai 11, 2024."

Mshukiwa alikamatwa Jumatatu asubuhi kutoka mafichoni huko Kayole.

Mshukiwa anakaa takriban mita 500 kutoka eneo la taka la Kware ambapo takriban miili kumi ya wanawake iliyoharibika vibaya ilipatikana katika operesheni.

Kulingana na Amin, pia alikiri kwamba mwathirika wake wa kwanza alikuwa mke wake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved