logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Itakuwa heshima kuhudumu kama Waziri wa Nishati - Wandayi

Anahudumu kwa muhula wake wa tatu bungeni baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza 2013

image

Habari24 July 2024 - 14:36

Muhtasari


  • “Itakuwa heshima kubwa na fahari kutumikia nchi yangu katika wadhifa huu mpya ikiwa nitapata idhini ya Bunge la Kitaifa. Shukrani zangu kwa Baba,” alisema.

Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi amesema kuwa itakuwa heshima kwake kuhudumu nchini kama Waziri wa Kawi na Nishati.

Katika ujumbe aliotuma kwenye X, Mbunge huyo wa Ugunja alimshukuru Rais William Ruto kwa kumteua kuwania nafasi hiyo Jumatano.

“Itakuwa heshima kubwa na fahari kutumikia nchi yangu katika wadhifa huu mpya ikiwa nitapata idhini ya Bunge la Kitaifa. Shukrani zangu kwa Baba,” alisema.

Wandayi pia alimshukuru kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kwa "kustahimili ushauri na malezi."

Wandayi sasa anatazamiwa kuchunguzwa na Bunge na iwapo ataidhinishwa atakuwa Waziri mpya atakayerithi mikoba ya Davis Chirchir ambaye ameteuliwa kuchukua ile ya Barabara iliyokuwa ikishikiliwa na Kipchumba Murkomen.

Anahudumu kwa muhula wake wa tatu bungeni baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza 2013 kwa tiketi ya ODM.

Eneo bunge la Ugunja lilitengwa na eneo bunge la Ugenya na kuifanya kuwa eneo bunge la sita katika kaunti ya Siaya.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved