logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu utajiri wa waliopendekezwa kuwa mawaziri ambao walipigwa msasa Agosti 1

Wakiwa mbele ya kamati hiyo, wateule wa baraza la mawaziri wote walihitajika kutangaza thamani yao ya sasa.

image
na Samuel Maina

Habari02 August 2024 - 05:37

Muhtasari


  • •Wakiwa mbele ya kamati hiyo, wateule wa baraza la mawaziri wote walihitajika kutangaza thamani yao ya sasa.
  • •Uhakiki wa walioteuliwa utaendelea kwa siku nne kuanzia Agosti 1, 2024 hadi Jumapili, Agosti 4, 2024.
walipigwa msasa Agosti 1, 2024.

Uhakiki wa wateule wa Baraza la Mawaziri ulianza Bungeni Alhamisi, Agosti 1, 2024.

Mteule wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Kithure Kindiki alikuwa wa kwanza kupigwa msasa na kamati kuhusu uteuzi.

Mteule huyo alifika katika Majengo ya Bunge dakika chache kabla ya saa mbili asubuhi. Uhakiki ulipangwa kuanza saa mbili asubuhi, hata hivyo, ulicheleweshwa na ulianza saa mbili unusu asubuhi.

Mteule wa Wizara ya Afya, Deborah Mulongo Barasa alikuwa wa pili kupigwa msasa na Kamati ya Uteuzi ya Bunge la Kitaifa.

Alice Wahome wa wizara ya ardhi alifuatwa mwendo wa saa sita adhuhuri , Migos Ogamba wa elimu akaingia saa tisa alasiri, na Soipan Tuya wa Ulinzi alifunga siku hiyo mwendo wa saa kumi na moja jioni.

Wakiwa mbele ya kamati hiyo, wateule wa baraza la mawaziri, waliohudumu katika baraza la mawaziri lililovunjwa na wale ambao wameteuliwa hivi majuzi, wote walihitajika kutangaza thamani yao ya sasa.

Hii hapa orodha ya thamani halisi iliyotangazwa na wateule mbalimbali;

  • Kithure Kindiki (Usalama wa Ndani), Sh544m, kutoka Sh694m mnamo Oktoba 2022.
  • Alice Wahome (Ardhi, kazi za umma), Sh327m kutoka Sh218m mnamo Oktoba 2022.
  • Soipan Tuya (Ulinzi), Sh243.4m, kutoka Sh156m mnamo Oktoba 2022.
  • Deborah Barasa (Afya), Sh455.8m
  • Julius Ogamba (Elimu), Sh790m

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa mwezi uliopita, uhakiki wa walioteuliwa utaendelea kwa siku nne, ambapo angalau wateule watano watapigwa msasa kuanzia Alhamisi, Agosti 1, 2024 hadi Jumapili, Agosti 4, 2024.

Mnamo Agosti 2, kamati itawapiga msasa  Andrew Mwihia (Kilimo) saa mbili asubuhi, Aden Duale (Mazingira) saa nne asubuhi, Eric Muuga (Maji), Davis Chirchir (Uchukuzi) na Margaret Ndung’u (ICT).

Mnamo Agosti 3, John Mbadi (Hazina), Salim Mvurya (Biashara), Rebecca Miano (Utalii) saa sita adhuhuri, Opiyo Wandayi (Nishati) saa tisa alasiri na Kipchumba Murkomen (Michezo) watatokea mbele ya  kamati ya uhakiki.

Mnamo Agosti 4, Hassan Joho (Madini), Alfred Mutua (Kazi), Wycliffe Oparanya (Ushirika), Justin Muturi (Utumishi wa Umma) na Stella Lang'at (Jinsia) watapigwa msasa..


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved