logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bunge la Bangladesh lavunjwa - Ofisi ya Rais

"Hadi usalama wa kila polisi utakapopatikana, tunatangaza mgomo," Mamlaka hiyo ilisema katika taarifa.

image
na Samuel Maina

Habari06 August 2024 - 11:24

Muhtasari


  • •Ilikuwa moja ya masharti yaliyotolewa na waratibu wa maandamano ya wanafunzi, ambao walikuwa wameweka makataa ya saa tisa.
wa Bangladesh walivamia ikulu na kumfanya waziri mkuu kujiuzulu.

Bunge la Bangladesh limevunjwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya rais.

Ilikuwa moja ya masharti yaliyotolewa na waratibu wa maandamano ya wanafunzi, ambao walikuwa wameweka makataa ya saa tisa (09:00 GMT).

Waandamanaji wa wanafunzi wamesema hawatakubali serikali inayoongozwa na jeshi, wakiongeza kuwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Muhammad Yunus amekubali kuwa mshauri mkuu wa serikali ya mpito.

Huku hayo yakijiri Chama cha Huduma ya Polisi ya Bangladesh (BPSA) kimesema kuwa maafisa wake wameanza mgomo.

"Hadi usalama wa kila polisi utakapopatikana, tunatangaza mgomo," Mamlaka hiyo ilisema katika taarifa.

BPSA ambayo inawakilisha maelfu ya maafisa wa polisi kote nchini. Ilisema kuwa zaidi ya vituo 450 vya polisi vilishambuliwa siku ya Jumatatu, katika maandamnao ya kumshinikiza Waziri Mkuu Sheikh Hasina kujiuzulu.

Maafisa kadhaa wa polisi pia waliuawa wakati wa maandamano hayo, kulingana na maafisa.

Idhaa ya BBC Bangla tayari ilikuwa imeripoti kuwa hakuna polisi wa trafiki wanaoonekana kwenye barabara nyingi katika mji mkuu wa Dhaka mapema Jumanne, huku wanafunzi wakionekana katika baadhi ya maeneo wakielekeza trafiki.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved