logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Similiki gari lililopatikana na vitoa machozi – Wanjigi

Mfanyibiashara Jimi Wanjigi amejitenga na gari ililokuwa na vitoa machozi.

image
na Davis Ojiambo

Habari09 August 2024 - 09:54

Muhtasari


  • • IG alimtaka Wanjigi kujisalimisha kwa polisi ili kuhojiwa.Wanjigi sasa anasema gari hilo si lake au la washirika wake kama ilivyoripotiwa awali. 
  • • Wanjigi ameiomba mahakama kumpa dhamana ya kutarajia dhidi ya hatua ya kukamatwa au kushtakiwa na polisi. 

Mfanyabiashara Jimmy Wanjigi amedai kuwa yeye si mmiliki wa gari linalodaiwa kupatikana na vitoa machozi wakati wa maandamano ya Nane Nane jijini Nairobi. 

Wanjigi katika kesi iliyowasilishwa katika Mahakama ya Milimani anasema anasingiziwa andaliwa kwa sababu za kisiasa. 

Katika kikao na wanahabari, kaimu Inspekta jenerali wa polisi Alhamisi alifahamisha umma kwamba walipata vitoa machozi vinne, chaja mbili za Motorola, simu moja ya miongoni mwa vifaa vingine kwenye gari lililoegeshwa kando ya lango la Wanjigi. 

Kutokana na kupatikana kwa vifaa hivyo, IG alimtaka Wanjigi kujisalimisha kwa polisi ili kuhojiwa.Wanjigi sasa anasema gari hilo si lake au la washirika wake kama ilivyoripotiwa awali. 

"Ninaamini kuwa IG hana sababu halali za kunikamata au kujiwasilisha kwenye kituo chochote cha polisi kama alivyodai au kupendekeza mashtaka ya jinai dhidi yangu," alisema. 

Kupitia kwa wakili Nelson Osiemo, Wanjigi ameiomba mahakama kumpa dhamana ya kutarajia dhidi ya hatua ya kukamatwa au kushtakiwa na polisi. Pia kinachotafutwa ni amri ya kumzuia IG kumkamata na kudhibiti haki zake kusafiri? 

"Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, nimekuwa nikipatwa na msongo wa mawazo na kisaikolojia kwani maafisa wa polisi wamekuwa wakinitisha, kuninyanyasa na kunifuata nyuma," alisema. 

Anasema ana uhuru na haki yake ya faragha imeminywa kwa kisingizio kuwa anafadhili maandamano kote nchini.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved