logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumamosi

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Uasin Gishu, na Bungoma.

image
na Samuel Maina

Habari10 August 2024 - 05:40

Muhtasari


  • •KPLC ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Agosti 10. 

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Uasin Gishu, na Bungoma.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za barabara ya Mombasa Road na Southern Bypass zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Chemtech Factory, Jua Kali na Mo Gas katika kaunti ya Uasin Gishu yataathirika kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za mji wa Webuye, Pan Paper na Law Courts katika kaunti ya Bungoma zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa nane alasiri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved